2 Corinthians 6:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msiambatane na watu wasioamini. Je, wema na uovu vyapatana kweli? Mwanga na giza vyawezaje kukaa pamoja?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini. Kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninyi hamko sawa na wale wasioamini. Hivyo msifungwe nira pamoja nao. Wema na ubaya havikai pamoja. Nuru na giza haviwezi kukaa pamoja katika chumba kimoja.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Msiambatane na watu wasioamini. Je, wema na uovu vyapatana kweli? Mwanga na giza vyawezaje kukaa pamoja?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msiambatane na watu wasioamini. Je, wema na uovu vyapatana kweli? Mwanga na giza vyawezaje kukaa pamoja?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msiambatane na watu wasioamini. Je, wema na uovu vyapatana kweli? Mwanga na giza vyawezaje kukaa pamoja?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Msiingie utumwa wa mwingine pamoja nao wasiomtegemea Mungu! Je? Yako magawio wongufu na upotovu unayoyagawiana? Au iko bia ya mwanga na ya giza?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musishirikiane pamoja na watu wasioamini. Kwa maana kuna ushirika gani kati ya haki na uovu? Kuna mapatano gani kati ya mwangaza na giza?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Msifungiwe kongwa pamoja na wasioamini, wasio na tabia kama zenu; kwa maana pana shirika gani kati ya haki na uasi? tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?