2 Corinthians 6:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha yetu kila upande.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
katika maneno ya kweli na katika nguvu za Mungu; kwa silaha za haki mkononi wa kuume na mkononi wa kushoto;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
kwa kusema iliyo kweli, na kwa kuzitegemea nguvu za Mungu. Njia hii iliyo sahihi ya kuishi imetuandaa kujitetea wenyewe kinyume na kila aina ya shambulizi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha yetu upande wa kulia na upande wa kushoto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha yetu kila upande.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
katika maneno ya kweli na katika nguvu za Mungu, kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
katika maneno ya kweli na katika nguvu za Mungu, kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kulia na za mkono wa kushoto;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha yetu kila upande.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
neno la kweli, nayo nguvu ya Mungu. Mata yanayotupa kushinda kuumeni na kushotoni ndiyo ya wongofu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
ya ujumbe wa neno la kweli, na ya uwezo wa Mungu. Tunatumia kama vile silaha mambo ya haki kwa kushambulia na kujikinga.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za wema za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto,