2 Corinthians 7:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuwa na huzuni jinsi atakavyo Mungu husababisha badiliko la moyo, badiliko lenye kuleta wokovu; hivyo hakuna sababu ya kujuta. Lakini huzuni ya kidunia huleta kifo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana huzuni ya kiungu huleta toba iletayo wokovu, wala haina majuto. Lakini huzuni ya kidunia husababisha mauti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Aina ya huzuni ambayo Mungu anaitaka inawafanya watu waamue kubadili maisha yao. Hili linawaelekeza kwenye wokovu, nasi hatuwezi kulijutia hilo. Lakini huzuni dunia huleta mauti.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kuwa na huzuni jinsi atakavyo Mungu, husababisha badiliko la moyo, badiliko lenye kuleta wokovu; hivyo hakuna sababu ya kujuta. Lakini huzuni ya kidunia huleta kifo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuwa na huzuni jinsi atakavyo Mungu husababisha badiliko la moyo, badiliko lenye kuleta wokovu; hivyo hakuna sababu ya kujuta. Lakini huzuni ya kidunia huleta kifo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana huzuni ya kimungu huleta toba iletayo wokovu na wala haina majuto. Lakini huzuni ya kidunia husababisha mauti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana huzuni ya kimungu huleta toba iletayo wokovu na wala haina majuto. Lakini huzuni ya kidunia husababisha mauti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba iletayo wokovu isiyo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuwa na huzuni jinsi atakavyo Mungu husababisha badiliko la moyo, badiliko lenye kuleta wokovu; hivyo hakuna sababu ya kujuta. Lakini huzuni ya kidunia huleta kifo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani sikitiko la Kimungu humpeleka mtu penye wokovu, likimpatia majuto yasiyojutika tena. Lakini sikitiko la kiulimwengu humpeleka mtu penye kufa.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, huzuni inayosababishwa na Mungu inamuwezesha mutu kugeuka toka katika zambi. Na kugeuka kule, kunamuletea kuokoka. Kule kuokoka hakuleti majuto. Lakini huzuni inayosababishwa na mwanadamu inaleta kifo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana huzuni iliyo mbele za Mungu hufanyiza toba iletayo wokofu isiyo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanyiza mauti.