2 Corinthians 7:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa mnaweza kuona matokeo ya kuona huzuni jinsi Mungu atakavyo: Nyinyi mmepata kuwa sasa watu wenye jitihada, wenye hoja, mnashtuka na kuogopa, mna bidii na mko tayari kuona kwamba haki yatekelezwa. Nyinyi mmethibitisha kwa kila njia kwamba hamna hatia kuhusu jambo hili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazameni jinsi huzuni hii ya kiungu ilivyoleta faida ndani yenu: bidii mliyo nayo, juhudi mliyofanya kujitetea, uchungu wenu, hofu yenu, upendo wenu, shauku yenu na jinsi mlivyokuwa tayari kutoa adhabu inayostahili. Kwa kila njia mmejithibitisha kuwa safi katika jambo hilo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko kwa jinsi ya Mungu kulitenda bidii kama nini ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na hofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi! Kwa kila njia mmejionyesha wenyewe kuwa safi katika jambo hilo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mlikuwa na huzuni ambayo Mungu alitaka muwe nayo. Sasa mmetambua kile ambacho huzuni hiyo imewaletea: Imewafanya muwe makini sana. Imewafanya mtafute kuthibitisha kuwa hamkufanya makosa. Iliwafanya mkasirike na mwogope. Imewafanya muwe na shauku ya kuniona. Imewafanya muwe na azma ya kufanya kile nilichowaagiza. Imewafanya muwe na shauku ya kuona kuwa haki inatendeka. Mlithibitisha kuwa hamkuwa na hatia katika sehemu yoyote ya tatizo hilo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sasa mnaweza kuona matokeo ya kuona huzuni jinsi Mungu atakavyo: ninyi mmepata kuwa sasa watu wenye jitihada, wenye hoja, mnashtuka na kuogopa, mna bidii na mko tayari kuona kwamba haki yatekelezwa. Ninyi mmethibitisha kwa kila njia kwamba hamna hatia kuhusu jambo hili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa mnaweza kuona matokeo ya kuona huzuni jinsi Mungu atakavyo: nyinyi mmepata kuwa sasa watu wenye jitihada, wenye hoja, mnashtuka na kuogopa, mna bidii na mko tayari kuona kwamba haki yatekelezwa. Nyinyi mmethibitisha kwa kila njia kwamba hamna hatia kuhusu jambo hili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazameni jinsi huzuni hii ya kimungu ilivyoleta faida ndani yenu: bidii mliyo nayo, juhudi mliyofanya kujitetea, uchungu wenu, hofu yenu, upendo wenu, shauku yenu na jinsi mlivyokuwa tayari kutoa adhabu inayostahili. Kwa kila njia mmethibitisha kuwa hamna hatia katika jambo hilo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazameni jinsi huzuni hii ya kimungu ilivyoleta faida ndani yenu: bidii mliyo nayo, juhudi mliyofanya kujitetea, uchungu wenu, hofu yenu, upendo wenu, shauku yenu na jinsi mlivyokuwa tayari kutoa adhabu inayostahili. Kwa kila njia mmejithibitisha kuwa safi katika jambo hilo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana, angalieni, kuhuzunishwa huko huko kwa jinsi ya Mungu kulitenda bidii gani ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na hofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi! Kwa kila njia mmejionesha wenyewe kuwa safi katika jambo hilo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa mnaweza kuona matokeo ya kuona huzuni jinsi Mungu atakavyo: Nyinyi mmepata kuwa sasa watu wenye jitihada, wenye hoja, mnashtuka na kuogopa, mna bidii na mko tayari kuona kwamba haki yatekelezwa. Nyinyi mmethibitisha kwa kila njia kwamba hamna hatia kuhusu jambo hili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani tazameni, kule kusikitishwa Kimungu kuko huko ndiko kulikowahimiza hivyo, mjikanie kwa kuona machukivu na woga, mkatunukia kulilipiza lile neno upesi. Mlipoyafanya hayo yote mmejitokeza wenyewe, ya kuwa hammo katika jambo lile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko kwa jinsi ya Mungu kulitenda bidii kama nini ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na hofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi! Kwa kila njia mmejionyesha wenyewe kuwa safi katika jambo hilo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, muangalie sasa matokeo ya ile huzuni inayosababishwa na Mungu! Imewafanya kuwa wenye bidii sana, wenye kujitetea, wenye kuonyesha kwamba hamuna kosa, wenye utii, wenye hamu kubwa ya kuniona, wenye kujitoa kwa ajili yangu na wenye kutaka kabisa kuazibu ubaya. Mumeonyesha katika njia zote kwamba hamukukuwa na kosa katika mambo haya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko mbele za Mungu kwalitenda bidii ya namna gani ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na khofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi. Kwa killa njia mmejionyesha kuwa safi katika jambo hilo.