2 Corinthians 7:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, ingawa niliandika ile barua, haikuwa kwa ajili ya yule aliyekosa, au kwa ajili ya yule aliyekosewa. Niliandika kusudi ionekane wazi mbele ya Mungu jinsi mlivyo na bidii kwa ajili yetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo, ingawa niliwaandikia, haikuwa kwa sababu ya huyo aliyekosa au huyo aliyekosewa. Lakini nilitaka ninyi wenyewe mwone mbele za Mungu jinsi mlivyojitoa kwa ajili yetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, ijapokuwa naliwaandikia, sikuandika kwa ajili yake yeye aliyedhulumu, wala si kwa ajili yake yeye aliyedhulumiwa, bali bidii yenu kwa ajili yetu ipate kudhihirishwa kwenu mbele za Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sababu kubwa ya kuandika barua ile haikuwa kwa sababu ya yule aliyefanya kosa au aliyeumia. Niliandika ili mtambue, mbele za Mungu, jinsi mnavyotujali sana sisi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivyo, ingawa niliandika ile barua, haikuwa kwa ajili ya yule aliyekosa, au kwa ajili ya yule aliyekosewa. Niliandika kusudi ionekane wazi mbele ya Mungu jinsi mlivyo na bidii kwa ajili yetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, ingawa niliandika ile barua, haikuwa kwa ajili ya yule aliyekosa, au kwa ajili ya yule aliyekosewa. Niliandika kusudi ionekane wazi mbele ya Mungu jinsi mlivyo na bidii kwa ajili yetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo ingawa niliwaandikia, haikuwa kwa sababu ya huyo aliyekosa au huyo aliyekosewa. Lakini nilitaka ninyi wenyewe mwone, mbele za Mungu, jinsi mlivyojitoa kwa ajili yetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo ingawa niliwaandikia, haikuwa kwa sababu ya huyo aliyekosa au huyo aliyekosewa. Lakini nilitaka ninyi wenyewe mwone, mbele za Mungu, jinsi mlivyojitoa kwa ajili yetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, ijapokuwa niliwaandikia, sikuandika kwa ajili yake yeye aliyedhulumu, wala si kwa ajili yake yeye aliyedhulumiwa, bali ili bidii yenu kwa ajili yetu ipate kudhihirishwa kwenu mbele za Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, ingawa niliandika ile barua, haikuwa kwa ajili ya yule aliyekosa, au kwa ajili ya yule aliyekosewa. Niliandika kusudi ionekane wazi mbele ya Mungu jinsi mlivyo na bidii kwa ajili yetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami hapo, nilipowaandikia, sikuandika kwa ajili yake aliyepotoa, wala kwa ajili yake aliyepotolewa, ila naliandikia kwamba: Kwenu kuonekane, ninyi mnavyojihimiza kwa ajili yetu mbele ya Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, ijapokuwa naliwaandikia, sikuandika kwa ajili yake yeye aliyedhulumu, wala si kwa ajili yake yeye aliyedhulumiwa, bali bidii yenu kwa ajili yetu ipate kudhihirishwa kwenu mbele za Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi ikiwa nimewaandikia, si kwa ajili ya yule aliyefanya kosa au si kwa ajili ya yule aliyemukosea. Lakini kusudi mupate kutambua waziwazi mbele ya Mungu bidii munayokuwa nayo kwa ajili yetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, ijapokuwa naliwaandikia, sikuandika kwa ajili yake yeye aliyedhulumu, wala si kwa ajili yake aliyedhulumiwa, bali ijtihadi yenu kwa ajili yetu ipate kudhihirishwa kwenu mbele za Mungu.