2 Corinthians 7:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi nimewasifu sana mbele yake, na katika jambo hilo sikudanganyika. Tumewaambieni ukweli daima, na kule kuwasifia nyinyi mbele ya Tito kumekuwa jambo la ukweli tupu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilikuwa nimewasifu ninyi kwake, nanyi hamkuniaibisha. Lakini kama vile yale yote tuliyowaambia yalikuwa kweli, hivyo kule kujisifu kwetu kwa Tito kuwahusu ninyi kumethibitishwa kuwa kweli pia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana, ikiwa nimejisifu mbele yake katika neno lo lote kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; bali, kama tulivyowaambia mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilijisifu juu yenu kwake Tito, na ninyi hamkuniaibisha. Siku zote tumewaambia ninyi kweli, na sasa yale tuliyomwambia Tito kwa habari zenu yamedhihirika kuwa ni kweli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mimi nimewasifu sana mbele yake, na katika jambo hilo sikudanganyika. Tumewaambieni ukweli daima, na kule kuwasifia ninyi mbele ya Tito kumekuwa jambo la ukweli mtupu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi nimewasifu sana mbele yake, na katika jambo hilo sikudanganyika. Tumewaambieni ukweli daima, na kule kuwasifia nyinyi mbele ya Tito kumekuwa jambo la ukweli tupu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilikuwa nimewasifu ninyi kwake, nanyi hamkuniaibisha. Lakini kila kitu tulichowaambia ninyi, kilikuwa kweli, hivyo kule kujisifu kwetu kwa Tito kuwahusu ninyi kumethibitishwa kuwa kweli pia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilikuwa nimewasifu ninyi kwake, nanyi hamkuniaibisha. Lakini kila kitu tulichowaambia ninyi, kilikuwa kweli, hivyo kule kujisifu kwetu kwa Tito kuwahusu ninyi kumethibitishwa kuwa kweli pia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana, ikiwa nimejisifu mbele yake katika neno lolote kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; bali, kama tulivyowaambia mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi nimewasifu sana mbele yake, na katika jambo hilo sikudanganyika. Tumewaambieni ukweli daima, na kule kuwasifia nyinyi mbele ya Tito kumekuwa jambo la ukweli tupu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama liko jambo la kwenu, nililojivunia kwake, halikunitokeza kuwa mwongo; lakini kama tulivyowaambia nanyi yote yaliyo ya kweli, vivyo hivyo hata yale, tuliyojivunia kwake Tito, yaliyokuwa ya kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana, ikiwa nimejisifu mbele yake katika neno lo lote kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; bali, kama tulivyowaambia mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi nimejivuna kidogo mbele yake kwa ajili yenu, nami sikupata haya. Lakini kama vile tulikuwa tunawaambia kila mara ukweli, vilevile kule kujisifu kwetu kwa ajili yenu mbele ya Tito, kumeonekana kuwa kwa kweli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana, ikiwa nimejisifu kwake kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; hali, kama tulivyowaambieni mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli.