2 Corinthians 7:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata baada ya kufika Makedonia hatukuweza kupumzika. Kila upande tulikabiliwa na taabu: Nje ugomvi; ndani hofu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana hata tulipoingia Makedonia, miili yetu haikuwa na amani. Tulisumbuliwa kila upande; kwa nje kulikuwa na mapigano, na mioyoni mwetu tulikuwa na hofu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tulidhikika kote kote; nje palikuwa na vita, ndani hofu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tulipokuja Makedonia, hatukupumzika. Tulisumbuliwa kwa kila namna. Tulikuwa na vita kwa nje na hofu ndani yetu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hata baada ya kufika Makedonia hatukuweza kupumzika. Kila upande tulikabiliwa na taabu: nje ugomvi; ndani hofu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata baada ya kufika Makedonia hatukuweza kupumzika. Kila upande tulikabiliwa na taabu: nje ugomvi; ndani hofu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana hata tulipoingia Makedonia, miili yetu haikuwa na raha. Tulisumbuliwa kila upande, kwa nje kulikuwa na mapigano na mioyoni mwetu tulikuwa na hofu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana hata tulipoingia Makedonia, miili yetu haikuwa na raha. Tulisumbuliwa kila upande, kwa nje kulikuwa na mapigano na mioyoni mwetu tulikuwa na hofu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tuliteseka kotekote; nje palikuwa na vita, ndani hofu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata baada ya kufika Makedonia hatukuweza kupumzika. Kila upande tulikabiliwa na taabu: Nje ugomvi; ndani hofu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani tulipofika Makedonia, miili yetu haikuweza kupumzikia kwa ajili ya maumivu yaliyotupata po pote, nje yalikuwako magombano, ndani mahangaiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tulidhikika kote kote; nje palikuwa na vita, ndani hofu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana hata wakati tulipofika Makedonia, hatukuweza kupumzika hata kidogo. Tulipata taabu pande zote: magomvi pamoja na watu wengine, na woga katika moyo wetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana hatta tulipokuwa tumelikia Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tuliteswa kote kote; nje palikuwa na vita, ndani khofu.