2 Corinthians 7:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa nafurahi, si kwa sababu mmehuzunika, ila kwa kuwa huzuni yenu imewafanya mbadili nia zenu na kutubu. Mmehuzunishwa kadiri ya mpango wa Mungu, na kwa sababu hiyo hatukuwadhuru nyinyi kwa vyovyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini sasa nina furaha, si kwa sababu mlihuzunika, bali kwa kuwa huzuni hiyo iliwafanya mtubu. Kwa maana mlihuzunishwa kama Mungu alivyokusudia watu wahuzunike, na hivyo sisi hatukuwadhuru kwa njia yoyote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sasa nafurahi, si kwa sababu ya ninyi kuhuzunishwa, bali kwa sababu mlihuzunishwa, hata mkatubu. Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu, ili msipate hasara kwa tendo letu katika neno lo lote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sasa ninafurahi, si kwa sababu mlipata huzuni, bali kwa sababu huzuni yenu iliwasababisha mkaamua kubadilika. Hilo ndilo ambalo Mungu alilitaka, hivyo hatukuwaumiza kwa namna yo yote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sasa nafurahi, si kwa sababu mmehuzunika, ila kwa kuwa huzuni yenu imewafanya mbadili nia zenu na kutubu. Mmehuzunishwa kadiri ya mpango wa Mungu, na kwa sababu hiyo hatukuwadhuru ninyi kwa vyovyote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa nafurahi, si kwa sababu mmehuzunika, ila kwa kuwa huzuni yenu imewafanya mbadili nia zenu na kutubu. Mmehuzunishwa kadiri ya mpango wa Mungu, na kwa sababu hiyo hatukuwadhuru nyinyi kwa vyovyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
lakini sasa nina furaha, si kwa sababu mlihuzunika, bali kwa kuwa huzuni hiyo iliwafanya mtubu. Kwa maana mlihuzunishwa kama Mungu alivyokusudia watu wahuzunike na hivyo sisi hatukuwadhuru kwa njia yo yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
lakini sasa nina furaha, si kwa sababu mlihuzunika, bali kwa kuwa huzuni hiyo iliwafanya mtubu. Kwa maana mlihuzunishwa kama Mungu alivyokusudia watu wahuzunike na hivyo sisi hatukuwadhuru kwa njia yoyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sasa nafurahi, si kwa sababu ya ninyi kuhuzunishwa, bali kwa sababu mlihuzunishwa, hata mkatubu. Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu, ili msipate hasara kwa tendo letu katika neno lolote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa nafurahi, si kwa sababu mmehuzunika, ila kwa kuwa huzuni yenu imewafanya mbadili nia zenu na kutubu. Mmehuzunishwa kadiri ya mpango wa Mungu, na kwa sababu hiyo hatukuwadhuru nyinyi kwa vyovyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
sasa nafurahi, si kwa sababu mmesikitishwa, ila kwa sababu masikitiko, mliyoyapata, yamewafundisha majuto. Kwani mmesikitishwa Kimungu, maana msiponzwe na jambo lo lote litokalo kwetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sasa nafurahi, si kwa sababu ya ninyi kuhuzunishwa, bali kwa sababu mlihuzunishwa, hata mkatubu. Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu, ili msipate hasara kwa tendo letu katika neno lo lote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa ninafurahi, si kwa sababu muliweza kuhuzunika, lakini kwa sababu huzuni yenu imewawezesha kugeuka toka katika zambi. Kwa maana mumehuzunishwa kufuatana na mupango wa Mungu. Kwa hivi hatukuwatendea ubaya wowote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sasa nafurahi, si kwa sababu ya kuhuzunishwa ninyi, bali kwa sababu mlihuzunishwa hatta mkatuhu. Maana mlihuzunishwa mmele za Mungu, msipate khasara kwa tendo letu katika neno lo lote.