2 Corinthians 8:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhusu jambo hili, basi, nawapeni shauri hili: Inafaa kwenu kutekeleza sasa yale mliyoanza mwaka jana. Nyinyi mlikuwa wa kwanza kuchukua hatua na kuamua kufanya hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ushauri wangu kuhusu lile lililo bora kwenu katika jambo hili ni huu: Mwaka uliopita ninyi mlikuwa wa kwanza si tu kutoa lakini pia mlikuwa na shauku ya kufanya hivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami katika neno hili natoa shauri langu; maana neno hili lawafaa ninyi mliotangulia, yapata mwaka, licha ya kutenda hata na kutaka pia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hili ndilo ninafikiri mnapaswa kufanya: mwaka jana mlikuwa wa kwanza kutaka kutoa, na mkawa wa kwanza kutoa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kuhusu jambo hili, basi, nawapeni shauri hili: inafaa kwenu kutekeleza sasa yale mliyoanza mwaka jana. Ninyi mlikuwa wa kwanza kuchukua hatua na kuamua kufanya hivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhusu jambo hili, basi, nawapeni shauri hili: inafaa kwenu kutekeleza sasa yale mliyoanza mwaka jana. Nyinyi mlikuwa wa kwanza kuchukua hatua na kuamua kufanya hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ushauri wangu kuhusu lile lililo bora kwenu juu ya jambo hili ni huu: Mwaka uliopita ninyi mlikuwa wa kwanza si tu kutoa lakini pia mlikuwa na shauku ya kufanya hivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ushauri wangu kuhusu lile lililo bora kwenu juu ya jambo hili ni huu: Mwaka uliopita ninyi mlikuwa wa kwanza si tu kutoa lakini pia mlikuwa na shauku ya kufanya hivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami katika neno hili natoa ushauri wangu; maana neno hili lawafaa ninyi mliotangulia, yapata mwaka, sio tu kutenda bali hata kutamani kutenda pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhusu jambo hili, basi, nawapeni shauri hili: Inafaa kwenu kutekeleza sasa yale mliyoanza mwaka jana. Nyinyi mlikuwa wa kwanza kuchukua hatua na kuamua kufanya hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami niliyoyatambua humu, ndiyo, ninayowatolea, kwani yanawafalia ninyi: mwaka wa jana mlitangulia kuifanya kazi hiyo; tena siko kuifanya tu, mlianza hata kuiitikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami katika neno hili natoa shauri langu; maana neno hili lawafaa ninyi mliotangulia, yapata mwaka, licha ya kutenda hata na kutaka pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuelekea jambo hilo, mimi ninawatolea shauri, nalo linafaa kwenu, kwa maana ni ninyi muliokuwa wa kwanza kukusudia kufanya kazi ile na kuianzisha tangu mwaka jana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nami katika neno hili natoa shauri langu; maana neno hili lawafaa ninyi mliotangulia, wapata mwaka, licha ya kutenda hivi, hatta kutaka pia.