2 Corinthians 8:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kamilisheni shughuli hiyo; na kama vile mlivyokuwa na hamu kubwa ya kusaidia, basi, fanyeni bidii vivyo hivyo, kadiri ya uwezo wenu, kuikamilisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa ikamilisheni kazi hii, ili shauku yenu ya kuitenda iandamane na kuimaliza, mkijitolea kulingana na uwezo wenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini sasa timizeni kule kutenda nako, ili kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo sasa ikamilisheni kazi mliyoianzisha. Kisha kutenda kwenu kutakuwa sawa na “kutaka” kwenu “kutenda”. Toeni kutokana na kile mlicho nacho.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, kamilisheni shughuli hiyo; na kama vile mlivyokuwa na hamu kubwa ya kusaidia, basi, fanyeni bidii vivyo hivyo, kadiri ya uwezo wenu, kuikamilisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kamilisheni shughuli hiyo; na kama vile mlivyokuwa na hamu kubwa ya kusaidia, basi, fanyeni bidii vivyo hivyo, kadiri ya uwezo wenu, kuikamilisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa ikamilisheni kazi hii kwa shauku kama mlivyoanza, jitoleeni kulingana na uwezo wenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa ikamilisheni kazi hii kwa shauku kama mlivyoanza, jitoleeni kulingana na uwezo wenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini sasa timizeni kule kutenda nako, ili kama vile mlivyokuwa tayari kutamani kutenda, vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kamilisheni shughuli hiyo; na kama vile mlivyokuwa na hamu kubwa ya kusaidia, basi, fanyeni bidii vivyo hivyo, kadiri ya uwezo wenu, kuikamilisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sasa sharti mmalize kuifanya, maana kama mapenzi yenu ya kuiitikia yalivyotokea upesi, vivyo hivyo mtokeze nayo mapenzi ya kuifanya mkichanga kwa vile, mlivyo navyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini sasa timizeni kule kutenda nako, ili kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa muendelee nayo na kuitimiza. Kama vile mulivyokuwa na moyo mwema wa kukusudia kuifanya, basi mukuwe na moyo mwema wa kuitimiza kufuatana na uwezo wa mali munayokuwa nayo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini sasa mkatimize kule kutenda nako, illi kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, vivyo hivyo mwe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo.