2 Corinthians 8:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi hampaswi kuongezewa taabu kusudi wengine wapunguziwe mzigo wao; sivyo, ila ni lazima tujali usawa na haki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nia yetu si kwamba wengine wasaidike wakati ninyi mnateseka, bali pawe na uwiano.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana sisemi hayo, ili wengine wapate raha nanyi mpate dhiki;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hatupendi muwe na mizigo wakati wengine wanastarehe. Tunataka kila kitu kiwe katika hali ya usawa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninyi hampaswi kuongezewa taabu kusudi wengine wapunguziwe mzigo wao; sivyo, ila ni lazima tujali usawa na haki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi hampaswi kuongezewa taabu kusudi wengine wapunguziwe mzigo wao; sivyo, ila ni lazima tujali usawa na haki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nia yetu si kwamba wengine wasaidike wakati ninyi mnateseka, bali pawe na uwiano.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nia yetu si kwamba wengine wasaidike wakati ninyi mnateseka, bali pawe na uwiano.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana sisemi hayo, ili wengine wapate raha nanyi mpate dhiki;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi hampaswi kuongezewa taabu kusudi wengine wapunguziwe mzigo wao; sivyo, ila ni lazima tujali usawa na haki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hatuchangii kwamba: Wengine wapate kutulia, ninyi mkiumizwa, ila sharti yalinganike:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana sisemi hayo, ili wengine wapate raha nanyi mpate dhiki;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nia yangu si kusema kwamba munapaswa kujitia katika taabu kwa ajili ya kusaidia watu wengine, lakini inafaa kuwe usawa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana sisemi haya, illi wengine waachiliwe ninyi mkalemewe,