2 Corinthians 8:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mlicho nacho sasa cha ziada kiwasaidie wale wanaohitaji, ili nao wakati watakapokuwa na ziada, wawasaidie nyinyi katika mahitaji yenu, na hivyo kuwe na usawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa wakati huu, wingi wa vitu mlivyo navyo utasaidia kutosheleza mahitaji yao, ili wakati wao watakapokuwa na wingi wa vitu, nao wapate kutosheleza mahitaji yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bali mambo yawe sawasawa; wakati huu wa sasa wingi wenu uwafae upungufu wao, ili na wingi wao uwafae ninyi mtakapopungukiwa; ili mambo yawe sawasawa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati huu mnavyo vingi na kuzidi na mnaweza kuwapa kila wanachohitaji. Kisha baadaye, watakapokuwa navyo vingi, wataweza kuwapa mnavyohitaji. Kisha kila mmoja atakuwa na mgao ulio sawa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kila mlicho nacho sasa cha ziada kiwasaidie wale wanaohitaji, ili nao wakati watakapokuwa na ziada, wawasaidie ninyi katika mahitaji yenu, na hivyo kuwe na usawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mlicho nacho sasa cha ziada kiwasaidie wale wanaohitaji, ili nao wakati watakapokuwa na ziada, wawasaidie nyinyi katika mahitaji yenu, na hivyo kuwe na usawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa wakati huu wingi wa vitu mlivyonavyo usaidie kutosheleza mahitaji yao, ili wakati wao wakiwa na wingi wa vitu, nao wapate kutosheleza mahitaji yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa wakati huu, wingi wa vitu mlivyo navyo usaidie kutosheleza mahitaji yao, ili wakati wao watakapokuwa na wingi wa vitu, nao wapate kutosheleza mahitaji yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bali mambo yawe sawasawa; wakati huu wa sasa wingi wenu uwafae upungufu wao, ili na wingi wao uwafae ninyi mtakapopungukiwa; ili mambo yawe sawasawa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mlicho nacho sasa cha ziada kiwasaidie wale wanaohitaji, ili nao wakati watakapokuwa na ziada, wawasaidie nyinyi katika mahitaji yenu, na hivyo kuwe na usawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mapato mengi yenu yao wale sharti yapunguze makosekano yenu ya siku nyingine; hivyo yatalinganika,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bali mambo yawe sawasawa; wakati huu wa sasa wingi wenu uwafae upungufu wao, ili na wingi wao uwafae ninyi mtakapopungukiwa; ili mambo yawe sawasawa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na sasa ninyi muko na mapato mengi zaidi, basi munaweza kuwasaidia wale wanaokuwa katika mahitaji. Hivi wao vilevile watakapokuwa na mapato mengi wataweza kuwasaidia katika siku za mahitaji. Kwa hiyo kutakuwa usawa
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bali mambo yawe sawa sawa: wakati huu wa sasa wingi wenu uwafae upungufu wao, illi na wingi wao uwafae ninyi upungufu wenu; illi mambo yawe sawa sawa.