2 Corinthians 8:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pamoja naye, tunamtuma ndugu mmoja ambaye sifa zake katika kueneza Injili zimeenea katika makanisa yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nasi tunamtuma pamoja naye ndugu ambaye anasifiwa na makundi yote ya waumini kwa huduma yake ya kuhubiri Injili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na pamoja naye tukamtuma ndugu yule ambaye sifa zake katika Injili zimeenea makanisani mwote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunamtuma Tito pamoja ndugu anayekubalika katika makanisa yote. Anasifiwa kwa sababu ya huduma yake ya Habari Njema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Pamoja naye, tunamtuma ndugu mmoja ambaye sifa zake katika kueneza Habari Njema zimeenea katika makanisa yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pamoja naye, tunamtuma ndugu mmoja ambaye sifa zake katika kueneza Injili zimeenea katika makanisa yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nasi tunamtuma pamoja naye ndugu ambaye anasifiwa na makanisa yote kwa huduma yake ya kuhubiri Injili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nasi tunamtuma pamoja naye ndugu ambaye anasifiwa na makundi yote ya waumini kwa huduma yake ya kuhubiri Injili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na pamoja naye tukamtuma ndugu yule ambaye sifa zake katika Injili zimeenea makanisani kote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pamoja naye, tunamtuma ndugu mmoja ambaye sifa zake katika kueneza Injili zimeenea katika makanisa yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tukatuma pamoja naye ndugu mmoja anayesifiwa kwenye wateule wote hivyo, anavyoutangaza Utume mwema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na pamoja naye tukamtuma ndugu yule ambaye sifa zake katika Injili zimeenea makanisani mwote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pamoja naye tunamutuma ndugu anayesifiwa na makanisa yote kwa ajili ya kazi yake ya kuhubiri Habari Njema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na pamoja nae tukamtuma ndugu yule ambae sifa zake katika Injili zimeenea makanisani mwote.