2 Corinthians 8:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zaidi ya hayo, yeye amechaguliwa na makanisa awe mwenzetu safarini wakati tunapopeleka huduma hii yetu ya upendo, huduma tunayoifanya kwa ajili ya utukufu wa Bwana na uthibitisho wa nia yetu njema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya hayo, alichaguliwa na makundi ya waumini ili asafiri pamoja nasi tulipokuwa tunapeleka matoleo ya ukarimu, kwa ajili ya utukufu wa Bwana Isa mwenyewe, na ili kuonesha hisani yetu kuwasaidia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala si hivyo tu, bali alichaguliwa na makanisa asafiri pamoja nasi katika jambo la neema hii, tunayoitumikia, ili Bwana atukuzwe, ukadhihirike utayari wetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pia, alichaguliwa na makanisa kuambatana nasi tunapoleta sadaka hii. Tunafanya huduma hii kumpa Bwana heshima na kuonesha kuwa tunapenda kusaidia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Zaidi ya hayo, yeye amechaguliwa na makanisa awe mwenzetu safarini wakati tunapopeleka huduma hii yetu ya upendo, huduma tunayoifanya kwa ajili ya utukufu wa Bwana na uthibitisho wa nia yetu njema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zaidi ya hayo, yeye amechaguliwa na makanisa awe mwenzetu safarini wakati tunapopeleka huduma hii yetu ya upendo, huduma tunayoifanya kwa ajili ya utukufu wa Bwana na uthibitisho wa nia yetu njema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya hayo, alichaguliwa na makanisa ili asafiri pamoja nasi tulipokuwa tunatoa huduma hii ya ukarimu kwa ajili ya utukufu wa Bwana mwenyewe ili kuonyesha hisani yetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya hayo, alichaguliwa na makundi ya waumini ili asafiri pamoja nasi tulipokuwa tunapeleka matoleo ya ukarimu, kwa ajili ya utukufu wa Bwana Isa mwenyewe, na ili kuonyesha hisani yetu kuwasaidia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala si hivyo tu, bali alichaguliwa na makanisa asafiri pamoja nasi katika jambo la neema hii, tunayoitumikia, ili Bwana atukuzwe, ukadhihirike utayari wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zaidi ya hayo, yeye amechaguliwa na makanisa awe mwenzetu safarini wakati tunapopeleka huduma hii yetu ya upendo, huduma tunayoifanya kwa ajili ya utukufu wa Bwana na uthibitisho wa nia yetu njema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sivyo hivyo tu, ila hata kuchaguliwa amechaguliwa nao wateule kuwa mfuasi wetu wa kutusaidia katika kazi hii ya vipaji, tutumikiayo sisi, tumtukuze Bwana, tukijulikana kuwa wenye kumpendeza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala si hivyo tu, bali alichaguliwa na makanisa asafiri pamoja nasi katika jambo la neema hii, tunayoitumikia, ili Bwana atukuzwe, ukadhihirike utayari wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile, yule ndugu amechaguliwa na makanisa kwa kutusindikiza katika safari ya kutimiza kazi hii ya kutoa kwa moyo mwema ambayo sisi tunafanya kwa ajili ya utukufu wa Bwana, na kwa kuonyesha nia yetu ya kusaidia watu wengine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wala si hivyo tu, bali alichaguliwa na makanisa asafiri pamoja nias katika jambo la neema hii inayokhudumiwa nasi, illi Bwana atukuzwe, ikadhihirike ya kuwa mioyo yenu ilikuwa tayari.