2 Corinthians 8:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tunataka kuepa lawama zinazoweza kutokea kuhusu usimamizi wetu juu ya zawadi hii karimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tunataka kuepuka lawama yoyote kuhusu jinsi tunavyosimamia matoleo haya ya ukarimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu kwa habari ya karama hii tunayoitumikia;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunajitahidi kuwa waangalifu ili asiwepo mtu wa kutukosoa kwa namna ambavyo tunashugulika na sadaka hii kubwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tunataka kuepa lawama zinazoweza kutokea kuhusu usimamizi wetu juu ya zawadi hii karimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tunataka kuepa lawama zinazoweza kutokea kuhusu usimamizi wetu juu ya zawadi hii karimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tunataka kuepuka lawama yo yote kuhusu jinsi tunavyosimamia matoleo haya ya ukarimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tunataka kuepuka lawama yoyote kuhusu jinsi tunavyosimamia matoleo haya ya ukarimu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu kuhusu karama hii tunayoitumikia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tunataka kuepa lawama zinazoweza kutokea kuhusu usimamizi wetu juu ya zawadi hii karimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo twajikinga, mtu asitusengenye kwa ajili ya machango haya makubwa yatumikiwayo nasi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu kwa habari ya karama hii tunayoitumikia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tunaepuka kushitakiwa na watu wengine juu ya mali mingi kama hii tunayochunga.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu katika khabari ya karama hii inayokhudumiwa nasi;