2 Corinthians 8:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nia yetu ni kufanya vema, si mbele ya Bwana tu, lakini pia mbele ya watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa tunakusudia kufanya kile kilicho haki, si machoni mwa Bwana Isa peke yake, bali pia machoni mwa wanadamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunajaribu kutenda lililo jema. Tunataka kufanya kile ambacho Bwana anakubali kuwa sahihi na kile ambacho watu wanafikiri kuwa ni sahihi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nia yetu ni kufanya vema, si tu mbele ya Bwana, lakini pia mbele ya watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nia yetu ni kufanya vema, si mbele ya Bwana tu, lakini pia mbele ya watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa tunakusudia kufanya kile kilicho haki si machoni mwa Bwana peke yake, bali pia machoni mwa watu wengine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa tunakusudia kufanya kile kilicho haki, si machoni mwa Bwana Isa peke yake, bali pia machoni mwa watu wengine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nia yetu ni kufanya vema, si mbele ya Bwana tu, lakini pia mbele ya watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani twajilindia, yaendelee vizuri, sipo mbele ya Bwana tu, ila napo mbele ya watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana tunataka kufanya mema, si mbele ya Bwana tu, lakini mbele ya watu vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele ya Bwana tu, bali na mbele ya wana Adamu.