2 Corinthians 8:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, pamoja na ndugu hao, tumemtuma ndugu yetu mwingine ambaye mara nyingi tumempa majaribio mbalimbali, tukamwona kuwa ni mwenye hamu kubwa ya kusaidia; hata sasa amekuwa na moyo zaidi kwa sababu ana imani sana nanyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pamoja nao, tunamtuma ndugu yetu ambaye mara kwa mara ametuthibitishia kwa njia nyingi kwamba ana shauku, naam, zaidi sana sasa kwa sababu analo tumaini kuu kwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nasi pamoja nao tumemtuma ndugu yetu tuliyemwona mara nyingi katika mambo mengi kuwa ana bidii, na sasa ana bidii zaidi sana kwa sababu ya tumaini kuu alilo nalo kwenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pia, tunawatuma pamoja nao kaka yetu ambaye yuko tayari siku zote kutoa msaada. Amethibitisha hili kwetu mara nyingi na kwa njia nyingi. Na anataka kusaidia zaidi sasa kwa sababu ana imani zaidi nanyi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, pamoja na ndugu hao, tumemtuma ndugu yetu mwingine ambaye mara nyingi tumempa majaribio mbalimbali, tukamwona kuwa ni mwenye hamu kubwa ya kusaidia; hata sasa amekuwa na moyo zaidi kwa sababu ana imani sana nanyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, pamoja na ndugu hao, tumemtuma ndugu yetu mwingine ambaye mara nyingi tumempa majaribio mbalimbali, tukamwona kuwa ni mwenye hamu kubwa ya kusaidia; hata sasa amekuwa na moyo zaidi kwa sababu ana imani sana nanyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pamoja nao, tunamtuma ndugu yetu ambaye mara kwa mara ametuthibitishia kwa njia nyingi kwamba ana shauku, naam, zaidi sana sasa kwa sababu analo tumaini kuu kwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pamoja nao, tunamtuma ndugu yetu ambaye mara kwa mara ametuthibitishia kwa njia nyingi kwamba ana shauku, naam, zaidi sana sasa kwa sababu analo tumaini kuu kwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nasi pamoja nao tumemtuma ndugu yetu tuliyemwona mara nyingi kuwa ana bidii katika mambo mengi, na sasa ana bidii zaidi sana kwa sababu ya tumaini kuu alilo nalo kwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, pamoja na ndugu hao, tumemtuma ndugu yetu mwingine ambaye mara nyingi tumempa majaribio mbalimbali, tukamwona kuwa ni mwenye hamu kubwa ya kusaidia; hata sasa amekuwa na moyo zaidi kwa sababu ana imani sana nanyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena pamoja nao tulituma ndugu yetu, tuliyemwona mara nyingi katika mambo mengi, anavyojihimiza. Lakini sasa anakaza kujihimiza, kwa sababu yako mengi, anayoyatazamia kwenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nasi pamoja nao tumemtuma ndugu yetu tuliyemwona mara nyingi katika mambo mengi kuwa ana bidii, na sasa ana bidii zaidi sana kwa sababu ya tumaini kuu alilo nalo kwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tunatuma ndugu yetu mwingine pamoja nao. Sisi tumemupima mara nyingi na ameonyesha siku zote kwamba yeye ni mwenye bidii sana. Na sasa, yeye ni mwenye bidii zaidi tena kwa kuwa anawaaminia ninyi sana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nasi pamoja nae tumemtuma ndugu yetu tuliyemwona katika mambo mengi kuwa ana bidii, na sasa ana bidii zaidi sana kwa sababu ya tumaini alilo nalo kwenu.