2 Corinthians 8:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tito ni mwenzangu; tunafanya kazi pamoja kwa ajili yenu; lakini kuhusu hawa ndugu zetu wengine wanaokuja pamoja nao, hao ni wajumbe wa makanisa, utukufu kwa Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa habari ya Tito, yeye ni mwenzangu na mtendakazi pamoja nami miongoni mwenu. Kwa habari za ndugu zetu, wao ni wawakilishi wa makundi ya waumini, na utukufu kwa Al-Masihi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mtu akitaka habari za Tito, yeye ni mshirika wangu, na mtenda kazi pamoja nami kwa ajili yenu; tena akitaka habari za ndugu zetu, wao ni mitume wa makanisa, na utukufu wa Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na sasa kuhusu Tito, yeye ni mshirika mwenzangu. Anafanya kazi pamoja nami kuwasaidia ninyi. Na kuhusu hawa kaka wawili wengine: wao wametumwa kutoka katika makanisa mengine, na wanaleta heshima kwa Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tito ni mwenzangu; tunafanya kazi pamoja kwa ajili yenu; lakini kuhusu hawa ndugu zetu wengine, wanaokuja pamoja nao, hao ni wajumbe wa makanisa, na utukufu kwa Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tito ni mwenzangu; tunafanya kazi pamoja kwa ajili yenu; lakini kuhusu hawa ndugu zetu wengine wanaokuja pamoja nao, hao ni wajumbe wa makanisa, utukufu kwa Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa habari ya Tito, yeye ni mwenzangu na mtenda kazi pamoja nami miongoni mwenu. Kwa habari za ndugu zetu, wao ni wawakilishi wa makanisa, na utukufu kwa Kristo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa habari ya Tito, yeye ni mwenzangu na mtendakazi pamoja nami miongoni mwenu. Kwa habari za ndugu zetu, wao ni wawakilishi wa makundi ya waumini, na utukufu kwa Al-Masihi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mtu akitaka habari za Tito, yeye ni mshirika wangu, na mtenda kazi pamoja nami kwa ajili yenu; tena akitaka habari za ndugu zetu, wao ni Mitume wa makanisa, na utukufu wa Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tito ni mwenzangu; tunafanya kazi pamoja kwa ajili yenu; lakini kuhusu hawa ndugu zetu wengine wanaokuja pamoja nao, hao ni wajumbe wa makanisa, utukufu kwa Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, Tito mwamjua kuwa mwenzangu anayenisaidia kazi za kwenu; nao hao ndugu zetu ni mitume wa wateule, maana wampatia Kristo utukufu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mtu akitaka habari za Tito, yeye ni mshirika wangu, na mtenda kazi pamoja nami kwa ajili yenu; tena akitaka habari za ndugu zetu, wao ni mitume wa makanisa, na utukufu wa Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa ngambo ya Tito, yeye ni mwenzangu, ninafanya kazi pamoja naye kwa ajili yenu. Nao wale wandugu wengine wanaomusindikiza, ni wajumbe wa makanisa wanaotumika kwa ajili ya utukufu wa Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi mtu akitaka khabari za Tito, yeye ni mshirika wangu, na mtenda kazi pamoja nami; tena akitaka khabari za ndugu zetu, wao ni mitume ya makanisa, na utukufu wa Kristo.