2 Corinthians 8:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, waonesheni uthabiti wa upendo wenu, makanisa yapate kuona kweli kwamba fahari ninayoona juu yenu ni ya halali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo waonesheni wazi hawa ndugu uthibitisho wa upendo wenu, na sababu inayotufanya tujivune kwa ajili yenu, ili makundi ya waumini yapate kuuona upendo wenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi waonyesheni mbele ya makanisa hakika ya upendo wenu, na ya kujisifu kwetu kwa ajili yenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo waonesheni watu hawa kuwa mna upendo. Waonesheni kwa nini tunajisifia ninyi. Ndipo makanisa yote yatakapo tambua hili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, waonyesheni uthabiti wa upendo wenu, makanisa yapate kuona kweli kwamba fahari ninayoona juu yenu ni ya halali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, waonesheni uthabiti wa upendo wenu, makanisa yapate kuona kweli kwamba fahari ninayoona juu yenu ni ya halali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo waonyesheni wazi hawa ndugu uthibitisho wa upendo wenu na sababu inayotufanya tujivune kwa ajili yenu, mbele ya makanisa, ili yapate kuona.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo waonyesheni wazi hawa ndugu uthibitisho wa upendo wenu na sababu inayotufanya tujivune kwa ajili yenu, mbele ya makundi ya waumini, ili yapate kuona.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi waonyesheni mbele ya makanisa hakika ya upendo wenu, na sababu ya kujisifu kwetu kwa ajili yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, waonesheni uthabiti wa upendo wenu, makanisa yapate kuona kweli kwamba fahari ninayoona juu yenu ni ya halali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, hao waonyesheni upendo wenu, tuliojivunia tulipowatukuza ninyi! Uonyesheni mbele yao wateule!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi waonyesheni mbele ya makanisa hakika ya upendo wenu, na ya kujisifu kwetu kwa ajili yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo muonyeshe mbele ya makanisa kwamba hakika munawapenda na kuyafahamisha kwamba tulikuwa na haki ya kujivuna kwa ajili yenu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi waonyesheni mbele ya makanisa bayana ya upendo wenu, na ya kujisifu kwetu kwa ajili yenu.