2 Corinthians 8:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi mna kila kitu: Imani, uwezo wa kusema, elimu; bidii yote ya kutenda mema, na upendo wenu kwetu. Hivyo, tunatazamia muwe wakarimu katika huduma hii ya upendo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kama vile mlivyo mbele sana katika yote, iwe ni katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika uaminifu wote na katika upendo wenu kwetu sisi, vivyo hivyo tunataka pia mzidi katika neema hii ya kutoa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kama mlivyo na wingi wa mambo yote; imani, na usemi, na elimu, na bidii yote, na upendo wenu kwetu sisi; basi vivyo hivyo mpate wingi wa neema hii pia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninyi ni matajiri kwa kila kitu; katika imani, katika uwezo wa kuzungumza, katika maarifa, katika utayari wa kusaidia kwa njia yo yote, na katika upendo mliojifunza kutoka kwetu. Hivyo sasa tunawataka muwe matajiri katika kazi hii ya kutoa pia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninyi mna kila kitu: imani, uwezo wa kusema, elimu; bidii yote ya kutenda mema, na upendo wenu kwetu. Hivyo, tunatazamia muwe wakarimu katika huduma hii ya upendo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi mna kila kitu: imani, uwezo wa kusema, elimu; bidii yote ya kutenda mema, na upendo wenu kwetu. Hivyo, tunatazamia muwe wakarimu katika huduma hii ya upendo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama vile mlivyo mbele sana katika yote: Katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika uaminifu wote na katika upendo wenu kwetu sisi, vivyo hivyo tunataka pia mzidi katika neema hii ya kutoa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama vile mlivyo mbele sana katika yote: Katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika uaminifu wote na katika upendo wenu kwetu sisi, vivyo hivyo tunataka pia mzidi katika neema hii ya kutoa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kama mlivyo na wingi wa mambo yote; imani, na usemi, na elimu, na bidii yote, na upendo wenu kwetu sisi; basi vivyo hivyo mpate wingi wa neema hii pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi mna kila kitu: Imani, uwezo wa kusema, elimu; bidii yote ya kutenda mema, na upendo wenu kwetu. Hivyo, tunatazamia muwe wakarimu katika huduma hii ya upendo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kama mwapitavyo wengine katika mambo yo yote, ikiwa kumtegemea Mungu au kupiga mbiu au kutaka utambuzi au kujihimiza kufanya mema yo yote au kutupenda kwa moyo, kama tunavyowapenda ninyi, hivyo sharti mwapite hata katika vipaji hivi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kama mlivyo na wingi wa mambo yote; imani, na usemi, na elimu, na bidii yote, na upendo wenu kwetu sisi; basi vivyo hivyo mpate wingi wa neema hii pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi munakuwa na kila kitu kwa uwingi: imani, usemi, ufahamu, kuwa na bidii ya kila namna na upendo munaokuwa nao kwetu. Kufuatana na hiyo mukuwe vilevile na uwingi katika kazi hii ya kuwa na moyo wa kutoa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini kama mlivyo na wingi wa vitu vyote, imani, na matamko, na elimu, na bidii yote, na mapenzi yenu kwetu sisi; bassi vivyo hivyo mwe na wingi wa neema hii pia.