2 Corinthians 9:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na Mungu ampaye mkulima mbegu na mkate kwa chakula, atawapa nyinyi pia mbegu mnazohitaji, na atazifanya ziote, zikue na kuwapa mavuno mengi ya ukarimu wenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye ampaye mpanzi mbegu ya kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa na kuzizidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu ndiye huwapa mbegu wale wanaopanda, na anatoa mkate kuwa chakula. Na Mungu atawapeni “mbegu” na kuifanya ile mbegu ikue. Atazalisha mazao makubwa kutokana na wema wenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na Mungu ampaye mkulima mbegu na mkate kwa chakula, atawapa ninyi pia mbegu mnazohitaji, na atazifanya ziote, ziwe na kuwapa mavuno mengi ya ukarimu wenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na Mungu ampaye mkulima mbegu na mkate kwa chakula, atawapa nyinyi pia mbegu mnazohitaji, na atazifanya ziote, zikue na kuwapa mavuno mengi ya ukarimu wenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye ampaye mpanzi mbegu kwa ajili ya kupanda na mkate kuwa chakula, atawapa na kuzizidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye ampaye mpanzi mbegu kwa ajili ya kupanda na mkate kuwa chakula, atawapa na kuzizidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na Mungu ampaye mkulima mbegu na mkate kwa chakula, atawapa nyinyi pia mbegu mnazohitaji, na atazifanya ziote, zikue na kuwapa mavuno mengi ya ukarimu wenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini yeye anayemtolea mpanzi mbegu hutoa nao mkate wa kula; yeye ataziongeza nazo mbegu zenu, ziwe nyingi, kisha atayachipuza mazao ya wongofu wenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu ndiye anayemupatia mupandaji mbegu na mukate wa kukula. Kwa hiyo atawapatia ninyi mbegu yoyote munayohitaji na kuiotesha, kusudi moyo wenu wa kutoa upate kuzaa matunda mengi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na yeye amruzukuye mbegu mwenye kupanda, atoae mkate uwe chakula, atawapeni mbegu za kupanda na kuzizidisha, atayaongeza mazao ya haki yenu;