2 Corinthians 9:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana huduma hii takatifu mnayoifanya si kwamba itasaidia mahitaji ya watu wa Mungu tu, bali pia itasababisha watu wengi wamshukuru Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huduma hii mnayofanya si tu ya kukidhi mahitaji ya watakatifu, bali huzidi sana kwa shukrani nyingi kwake Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Huduma mnayoitoa inawasaidia watu wa Mungu katika mahitaji yao, lakini si hayo tu itendayo. Inaleta pia shukrani nyingi zaidi na zaidi kwa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana huduma hii takatifu mnayoifanya si tu kwamba itasaidia mahitaji ya watu wa Mungu, bali pia itasababisha watu wengi wamshukuru Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana huduma hii takatifu mnayoifanya si kwamba itasaidia mahitaji ya watu wa Mungu tu, bali pia itasababisha watu wengi wamshukuru Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huduma hii mnayofanya si tu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watakatifu, bali huzidi sana kwa shukrani nyingi apewazo Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huduma hii mnayofanya si tu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watakatifu, bali huzidi sana kwa shukrani nyingi apewazo Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana huduma hii takatifu mnayoifanya si kwamba itasaidia mahitaji ya watu wa Mungu tu, bali pia itasababisha watu wengi wamshukuru Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kazi hii ya kuchanga vipaji, tunayoitumikia, siyo ya kuyaondoa tu mapungufu ya watakatifu, ila kupita hapo inatimilika kwao wengi, wakimtolea Mungu vipaji vya kumshukuru.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana kazi hii ya kutoa munayofanya haifai tu kwa kusaidia watu wa Mungu kusudi wapate vitu wanavyokosa, lakini vilevile kwa njia ile watu wengi wanamutolea Mungu shukrani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana utumishi wa khuduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu;