2 Corinthians 9:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutokana na uthibitisho unaooneshwa kwa huduma hii yetu, watu watamtukuza Mungu kwa sababu ya uaminifu wenu kwa Habari Njema ya Kristo mnayoiungama, na pia kwa sababu ya ukarimu mnaowapa wao na watu wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utiifu ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Al-Masihi, na kwa ukarimu wenu wa kuwashirikisha wao na watu wengine wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Huduma hii ni uthibitisho wa imani yenu, na watu watamsifu Mungu kwa sababu kwa uhuru mlitoa mkawapa sehemu pamoja na watu wengine pia. Watamsifu Mungu kwa sababu wanaona jinsi mnavyoifuata injili ya Yesu Kristo ambayo mliipokea kwa wazi kabisa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kutokana na uthibitisho unaoonyeshwa kwa huduma hii yetu, watu watamtukuza Mungu kwa sababu ya uaminifu wenu kwa Habari Njema ya Kristo mnayoiungama, na pia kwa sababu ya ukarimu mnaowapa wao na watu wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutokana na uthibitisho unaooneshwa kwa huduma hii yetu, watu watamtukuza Mungu kwa sababu ya uaminifu wenu kwa Habari Njema ya Kristo mnayoiungama, na pia kwa sababu ya ukarimu mnaowapa wao na watu wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utii ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Kristo na kwa ukarimu wenu wa kushiriki pamoja nao na pia wengine wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utiifu ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Al-Masihi, na kwa ukarimu wenu wa kushiriki pamoja nao na pia wengine wote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutokana na uthibitisho unaooneshwa kwa huduma hii yetu, watu watamtukuza Mungu kwa sababu ya uaminifu wenu kwa Habari Njema ya Kristo mnayoiungama, na pia kwa sababu ya ukarimu mnaowapa wao na watu wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kazi hii, tunayoitumikia, ikijulikana kuwa ya upendo wa kweli, watamtukuza Mungu, maana mmeyatii hayo, mnayoyaungama kuwa Utume mwema wa Kristo, nayo mioyo yenu ikajulika kwao kuwa yenye neno moja tu kwa hivyo, mlivyowagawia hao nao wengine wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kufuatana na ushuhuda wa kazi hii, watu watamutukuza Mungu kwa kuona jinsi munavyoonyesha utii wenu katika kushika Habari Njema ya Kristo. Vilevile wanamutukuza kwa kuona moyo wa kutoa munaokuwa nao katika kushirikiana mali yenu pamoja nao na sisi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huu, mnamtukuza Mungu kwa ajili ya ntii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.