2 Corinthians 9:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, nimeona ni lazima kuwaomba hawa ndugu watutangulie kuja kwenu, wapate kuweka tayari zawadi yenu kubwa mliyoahidi; nayo ioneshe kweli kwamba ni zawadi iliyotolewa kwa hiari na si kwa kulazimishwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hivyo niliona ni muhimu niwahimize hawa ndugu watangulie kuja huko kwenu kabla yangu, wafanye mipango ya hayo matoleo ya ukarimu mliyokuwa mmeahidi, ili yawe tayari kama matoleo ya hiari wala si kama ya kutozwa kwa nguvu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi naliona ya kuwa ni lazima niwaonye ndugu hawa watangulie kufika kwenu, na kutengeneza mapema karama yenu mliyoahidi tangu zamani, ili iwe tayari, na hivi iwe kama kipawa, wala si kama kitu kitolewacho kwa unyimivu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo nikafikiri kuwa niwaombe ndugu hawa waje kwenu kabla ya mimi kuja. Wao watasaidia kufanya maandalizi mapema kwa ajili ya sadaka yenu yenye ukarimu mliyoahidi. Kisha sadaka hii itakuwa tayari tutakapokuja, na itaonekana kuwa baraka, na si kitu kidogo ambacho hamkutaka kutoa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa hiyo, nimeona ni lazima kuwaomba hawa ndugu watutangulie kuja kwenu, wapate kuweka tayari zawadi yenu kubwa mliyoahidi; nayo ionyeshe kweli kwamba ni zawadi iliyotolewa kwa hiari na si kwa kulazimishwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, nimeona ni lazima kuwaomba hawa ndugu watutangulie kuja kwenu, wapate kuweka tayari zawadi yenu kubwa mliyoahidi; nayo ioneshe kweli kwamba ni zawadi iliyotolewa kwa hiari na si kwa kulazimishwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hivyo niliona ni muhimu niwahimize hawa ndugu watangulie kuja huko kwenu kabla yangu, wafanye mipango ya hayo matoleo ya ukarimu mliyokuwa mmeahidi, ili yawe tayari kama matoleo ya hiari wala si kama ya kutozwa kwa nguvu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hivyo niliona ni muhimu niwahimize hawa ndugu watangulie kuja huko kwenu kabla yangu, wafanye mipango ya hayo matoleo ya ukarimu mliyokuwa mmeahidi, ili yawe tayari kama matoleo ya hiari wala si kama ya kutozwa kwa nguvu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi niliona ya kuwa ni lazima niwaonye ndugu hawa watangulie kufika kwenu, na kutengeneza mapema karama yenu mliyoahidi tangu zamani, ili iwe tayari, na hivi iwe kama kipawa, wala si kama kitu kitolewacho kwa nguvu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, nimeona ni lazima kuwaomba hawa ndugu watutangulie kuja kwenu, wapate kuweka tayari zawadi yenu kubwa mliyoahidi; nayo ioneshe kweli kwamba ni zawadi iliyotolewa kwa hiari na si kwa kulazimishwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo nalijishurutisha kuwaonya ndugu waliotangulia kufika kwenu, waanze kuvichanga vipaji vya upendo wenu, mlivyotuagia kale, tuvikute, vimekwisha kuchangwa kuwa vipaji vya upendo wa kweli, sivyo vya choyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi naliona ya kuwa ni lazima niwaonye ndugu hawa watangulie kufika kwenu, na kutengeneza mapema karama yenu mliyoahidi tangu zamani, ili iwe tayari, na hivi iwe kama kipawa, wala si kama kitu kitolewacho kwa unyimivu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni hivi niliona kuwa ni vizuri kuwashauri wandugu hawa watangulie kufika kwenu mbele yangu kusudi watayarishe vile vitu mulivyoahidi kutoa kwa mapenzi yenu. Hivi vitakuwa tayari na itaonyesha kwamba mumevitoa kwa moyo mwema, wala si kwa uchoyo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi naliona ya kuwa ni lazima niwaonye ndugu hawa watangulie kufika kwenu, na kutengeneza mapema karama yenu mliyoahidi tangu zamani, illi iwe tayari, na hivi iwe kama kipawa, wala si kama kitu kitolewacho kwa choyo.