2 Corinthians 9:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu anaweza kuwapeni nyinyi zaidi ya yale mnayoyahitaji, mpate daima kuwa na kila kitu mnachohitaji, na hivyo mzidi kusaidia katika kila kazi njema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na Mungu anaweza kuwapeni baraka zaidi kuliko mlivyo katika kuhitaji kwenu, na daima mtakuwa na kila kitu mnachokihitaji. Mtakuwa na vingi vya ziada vya kutoa kwa kila kazi njema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu anaweza kuwapeni ninyi zaidi ya yale mnayoyahitaji, mpate daima kuwa na kila kitu mnachohitaji, na hivyo mzidi kusaidia katika kila kazi njema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu anaweza kuwapeni nyinyi zaidi ya yale mnayoyahitaji, mpate daima kuwa na kila kitu mnachohitaji, na hivyo mzidi kusaidia katika kila kazi njema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati, mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati, mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu anaweza kuwapeni nyinyi zaidi ya yale mnayoyahitaji, mpate daima kuwa na kila kitu mnachohitaji, na hivyo mzidi kusaidia katika kila kazi njema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Mungu anaweza kuwapatia matunzo yote, kwamba hayo, mpaswayo nayo, siku zote yawatoshee kabisa, tena yasalie ya kutolea kazi njema zote,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na Mungu anaweza kuwajalia mema ya kila namna, kusudi siku zote mupate vyote munavyohitaji, na hivi mupate kuzidi kutoshelewa katika kutenda kazi njema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Mungu aweza kuwajaza killa neema kwa wingi, illl ninyi, mkiwa na riziki za killa namna siku zote, mpate kuzidi sana katika killa tendo jema;