2 John 1:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ninayo mengi ya kuwaambieni, lakini sipendi kufanya hivyo kwa karatasi na wino; badala yake, natumaini kuwatembeleeni na kuzungumza nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ikamilike.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninayo mengi ya kuwaandikia, lakini sitaki kutumia karatasi na wino. Badala yake, nataraji kuja kwenu na kuongea nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraji kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe imetimizwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nina mengi ya kuwaambia. Lakini sitaki kutumia karatasi na wino. Badala yake, nataraji kuja kuwatembelea. Kisha tunaweza kujumuika pamoja na kuzungumza uso kwa uso. Ndipo furaha yetu itakamilika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninayo mengi ya kuwaambieni lakini sipendi kufanya hivyo kwa karatasi na wino; badala yake, natumaini kuwatembeleeni na kuzungumza nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ikamilike.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ninayo mengi ya kuwaambieni, lakini sipendi kufanya hivyo kwa karatasi na wino; badala yake, natumaini kuwatembeleeni na kuzungumza nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ikamilike.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa ninayo mengi ya kuwaandikia, lakini sitaki kutumia karatasi na wino. Badala yake, nataraji kuja kwenu na kuongea nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninayo mengi ya kuwaandikia, lakini sitaki kutumia karatasi na wino. Badala yake, nataraji kuja kwenu na kuongea nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini natarajia kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe imetimizwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ninayo mengi ya kuwaambieni, lakini sipendi kufanya hivyo kwa karatasi na wino; badala yake, natumaini kuwatembeleeni na kuzungumza nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ikamilike.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninayo mengi ya kuwaandikia ninyi, lakini sikutaka kuyamaliza kwa karatasi na wino, ila nangojea kwamba: Nitakuja kwenu na kusema nanyi kinywa kwa kinywa, furaha yetu itimie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraji kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe imetimizwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nina maneno mengi ya kuwaambia, lakini sitaki kuyaandika ndani ya barua. Ninatumaini nitawatembelea na kusemezana pamoja nanyi uso kwa uso, kusudi tupate kujazwa na furaha kabisa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa kuwa nina maneno mengi ya kuwa-andikia, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraja kuja kwenu, na kusema nanyi mdo-mo kwa mdomo, illi furaha yenu itimizwe.