2 Kings 1:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme akamtuma kapteni mwingine na watu wake hamsini wamlete Elia. Naye akapanda juu akamwambia Elia, “Ewe mtu wa Mungu, mfalme anakuamuru ushuke mara moja!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Aliposikia hili, mfalme akatuma kwa Ilya mkuu wa kikosi mwingine na askari wake hamsini. Yule mkuu wa kikosi akamwambia Ilya, “Mtu wa Mungu, hili ndilo asemalo mfalme, ‘Shuka chini mara moja!’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akatuma tena akida wa hamsini mwingine pamoja na hamsini wake, wamwendee. Akajibu, akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka upesi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme akamtuma kapteni mwingine na watu wake hamsini wamlete Elia. Naye akapanda juu akamwambia Elia, “Ewe mtu wa Mungu, mfalme anakuamuru ushuke mara moja!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika hili, mfalme akatuma kwa Eliya mkuu wa kikosi mwingine na askari wake hamsini. Yule mkuu wa kikosi akamwambia Eliya, “Mtu wa Mungu, hili ndilo asemalo mfalme, ‘Shuka chini mara moja!’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Aliposikia hili, mfalme akatuma kwa Ilya mkuu wa kikosi mwingine na askari wake hamsini. Yule mkuu wa kikosi akamwambia Ilya, “Mtu wa Mungu, hili ndilo asemalo mfalme, ‘Shuka chini mara moja!’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akatuma tena kiongozi wa hamsini mwingine pamoja na hamsini wake, wamwendee. Akajibu, akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka upesi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme akamtuma kapteni mwingine na watu wake hamsini wamlete Elia. Naye akapanda juu akamwambia Elia, “Ewe mtu wa Mungu, mfalme anakuamuru ushuke mara moja!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akatuma tena kwake mkuu mwingine wa kikosi cha hamsini na watu wake hamsini, naye akasema na kumwambia: Mtu wa Mungu, ndivyo, mfalme anavyosema: Shuka upesi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akatuma tena akida wa hamsini mwingine pamoja na hamsini wake, wamwendee. Akajibu, akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka upesi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme akamutuma kiongozi mwingine na watu wake makumi tano wamulete Elia. Naye akamwambia Elia: “Ewe mutu wa Mungu, mufalme anakuamuru ushuke mara moja!”