2 Kings 1:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa mara nyingine tena, mfalme akatuma kapteni mwingine na watu wake hamsini. Kapteni wa tatu akapanda mlimani, akapiga magoti mbele ya Elia na kumsihi akisema, “Ewe mtu wa Mungu, nakusihi uyathamini maisha yangu, na ya watu wako hawa, usituangamize!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo mfalme akatuma mkuu wa kikosi wa tatu na watu wake hamsini. Huyu mkuu wa kikosi wa tatu akapanda na kupiga magoti mbele ya Ilya, akiomba, “Mtu wa Mungu, tafadhali niachie uhai wangu na uhai wa hawa watu hamsini, watumishi wako!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena akatuma akida wa hamsini wa tatu, pamoja na hamsini wake. Yule akida wa hamsini wa tatu akapanda, akaenda akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana, akamwambia, Ee mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako hawa hamsini, ziwe na thamani machoni pako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa mara nyingine tena, mfalme akatuma kapteni mwingine na watu wake hamsini. Kapteni wa tatu akapanda mlimani, akapiga magoti mbele ya Elia na kumsihi akisema, “Ewe mtu wa Mungu, nakusihi uyathamini maisha yangu, na ya watu wako hawa, usituangamize!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo mfalme akatuma mkuu wa kikosi wa tatu na watu wake hamsini. Huyu mkuu wa kikosi wa tatu akapanda na kupiga magoti mbele ya Eliya, akiomba, “Mtu wa Mungu, tafadhali niachie uhai wangu na uhai wa hawa watu hamsini, watumishi wako!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo mfalme akatuma mkuu wa kikosi wa tatu na watu wake hamsini. Huyu mkuu wa kikosi wa tatu akapanda na kupiga magoti mbele ya Ilya, akiomba, “Mtu wa Mungu, tafadhali niachie uhai wangu na uhai wa hawa watu hamsini, watumishi wako!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena akatuma kamanda wa hamsini wa tatu, pamoja na hamsini wake. Yule kamanda wa hamsini wa tatu akapanda, akaenda akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana, akamwambia, Ee mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako hawa hamsini, ziwe na thamani machoni pako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa mara nyingine tena, mfalme akatuma kapteni mwingine na watu wake hamsini. Kapteni wa tatu akapanda mlimani, akapiga magoti mbele ya Elia na kumsihi akisema, “Ewe mtu wa Mungu, nakusihi uyathamini maisha yangu, na ya watu wako hawa, usituangamize!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akatuma mara ya tatu mkuu wa kikosi cha hamsini na watu wake hamsini; huyu mkuu wa tatu wa kikosi cha hamsini alipopanda na kufika kwake akampigia Elia magoti, akamwambia na kumbembeleza: Mtu wa Mungu, roho yangu nazo roho za hawa watumishi wako hamsini usiziwazie kuwa si kitu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena akatuma akida wa hamsini wa tatu, pamoja na hamsini wake. Yule akida wa hamsini wa tatu akapanda, akaenda akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana, akamwambia, Ee mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako hawa hamsini, ziwe na thamani machoni pako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mara ingine tena, mufalme akatuma kiongozi mwingine na watu wake makumi tano. Kiongozi wa tatu akapanda kwenye mulima, akapiga magoti mbele ya Elia na kumusihi akisema: “Ewe mutu wa Mungu, ninakusihi uyahesabu maisha yangu na maisha ya hawa watumishi wako makumi tano yakuwe ya bei kali mbele yako.