2 Kings 1:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akamwambia, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Kwa sababu ulituma wajumbe kumtaka shauri Baal-zebubu, mungu wa Ekroni — kana kwamba hapakuwa na Mungu katika Israeli ambaye ungemwomba shauri — basi, hutashuka katika kitanda ulichopanda; hakika utakufa.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamwambia mfalme, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli wa kumuuliza habari, ndiyo maana ukatuma wajumbe kuuliza Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni? Kwa sababu umefanya hili, kamwe hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwambia, Bwana asema hivi, Kwa kuwa umetuma wajumbe waulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, uulize neno lake? Kwa hiyo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akamwambia, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Kwa sababu ulituma wajumbe kumtaka shauri Baal-zebubu, mungu wa Ekroni — kana kwamba hapakuwa na Mungu katika Israeli ambaye ungemwomba shauri — basi, hutashuka katika kitanda ulichopanda; hakika utakufa.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamwambia mfalme, “Hili ndilo asemalo BWANA: Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli wa wewe kumwuliza ndiyo maana ukatuma wajumbe kuuliza Baal-Zebubu, aliye mungu wa Ekroni? Kwa sababu umefanya hili, kamwe hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia, Hakika utakufa!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamwambia mfalme, “Hili ndilo asemalo bwana: Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli wa kumuuliza habari, ndiyo maana ukatuma wajumbe kuuliza Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni? Kwa sababu umefanya hili, kamwe hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwambia, BWANA asema hivi, Kwa kuwa umetuma wajumbe waulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, je! Ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli, uulize neno lake? Kwa hiyo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akamwambia, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: ‘Kwa sababu ulituma wajumbe kumtaka shauri Baal-zebubu, mungu wa Ekroni – kana kwamba hapakuwa na Mungu katika Israeli ambaye ungemwomba shauri – basi, hutashuka katika kitanda ulichopanda; hakika utakufa.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamwambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa kuwa umetuma wajumbe kumwuliza Baali-Zebubu, mungu wa Ekroni, kama hakuna Mungu kwao Waisiraeli wa kumwuliza, atakavyosema, kwa sababu hii hutaondoka tena hapa kitandani, unapolala, ila utakufa kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwambia, BWANA asema hivi, Kwa kuwa umetuma wajumbe waulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, uulize neno lake? Kwa hiyo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akamwambia mufalme: “Yawe anasema hivi: ‘Kwa sababu ulituma wajumbe kuomba shauri kwa Bali-Zabubu mungu wa Ekuroni sawa vile hakuna Mungu katika Israeli ambaye ungemwomba shauri, basi, hautashuka katika kitanda ambacho umepanda juu yake. Hakika utakufa.’ ”