2 Kings 1:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye Ahazia akafariki kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia nabii wake Elia. Na, kwa kuwa Ahazia hakuwa na mtoto wa kiume, Yoramu akawa mfalme mahali pake, katika mwaka wa pili wa utawala wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati, mfalme wa Yuda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo akafa, sawasawa na lile neno la Mwenyezi Mungu ambalo Ilya alikuwa amesema. Kwa kuwa Ahazia hakuwa na mwana, Yoramu akawa mfalme baada yake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akafa, sawasawa na neno la Bwana alilolinena Eliya. Na Yoramu
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye Ahazia akafariki kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia nabii wake Elia. Na, kwa kuwa Ahazia hakuwa na mtoto wa kiume, Yoramu akawa mfalme mahali pake, katika mwaka wa pili wa utawala wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati, mfalme wa Yuda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo akafa, sawasawa na lile neno la BWANA ambalo Eliya alikuwa amesema. Kwa kuwa Ahazia hakuwa na mwana, Yoramu akaingia mahali pake kuwa mfalme katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo akafa, sawasawa na lile neno la bwana ambalo Ilya alikuwa amesema. Kwa kuwa Ahazia hakuwa na mwana, Yoramu akawa mfalme baada yake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akafa, sawasawa na neno la BWANA alilolinena Eliya. Na Yoramu alianza kutawala mahali pake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda; kwa kuwa yeye hakuwa na mwana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye Ahazia akafariki kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia nabii wake Elia. Na, kwa kuwa Ahazia hakuwa na mtoto wa kiume, Yoramu akawa mfalme mahali pake, katika mwaka wa pili wa utawala wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati, mfalme wa Yuda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akafa, kwa hilo neno la Bwana, Elia alilolisema; kisha Yoramuakawa mfalme mahali pake katika mwaka wa pili wa Yoramu, mwana wa Yosafati, mfalme wa Wayuda, kwani Ahazia hakuwa na mwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akafa, sawasawa na neno la BWANA alilolinena Eliya. Na Yoramu alianza kutawala mahali pake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda; kwa kuwa yeye hakuwa na mwana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Ahazia akakufa kama vile Yawe alivyomwambia nabii wake Elia. Na kwa sababu Ahazia hakukuwa na mutoto mwanaume, Yoramu akakuwa mufalme kwa pahali pake, katika mwaka wa pili wa utawala wa Yehoramu mwana wa Yosafati, mufalme wa Yuda.