2 Kings 1:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Ahazia alipokuwa Samaria alianguka kutoka chumba kilichokuwa paani mwa nyumba yake, akaumia vibaya. Kwa hiyo akawatuma wajumbe, akawaambia, “Nendeni kwa Baal-zebubu, mungu wa mji wa Ekroni, mkamwulize kama nitapona ugonjwa huu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Ahazia alikuwa ameanguka huko Samaria kutoka baraza ya chumba chake cha juu, akaumia. Hivyo akatuma wajumbe, akiwaambia, “Nendeni mkaulize kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni, mkaone kama nitapona kutokana na kuumia huku.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Ahazia akaanguka katika dirisha la chumba chake orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Ahazia alipokuwa Samaria alianguka kutoka chumba kilichokuwa paani mwa nyumba yake, akaumia vibaya. Kwa hiyo akawatuma wajumbe, akawaambia, “Nendeni kwa Baal-zebubu, mungu wa mji wa Ekroni, mkamwulize kama nitapona ugonjwa huu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Ahazia alikuwa ameanguka huko Samaria kutoka baraza ya chumba chake cha juu akaumia. Hivyo akatuma wajumbe, akiwaambia, “Nendeni mkaulize kwa Baal-Zebubu, aliye mungu wa Ekroni, mkaone kama nitapona kutokana na kuumia huku.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Ahazia alikuwa ameanguka huko Samaria kutoka baraza ya chumba chake cha juu, akaumia. Hivyo akatuma wajumbe, akiwaambia, “Nendeni mkaulize kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni, mkaone kama nitapona kutokana na kuumia huku.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Ahazia akaanguka kutoka dirisha la chumba chake ghorofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Nendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kama nitapona ugonjwa huu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Ahazia alipokuwa Samaria alianguka kutoka chumba kilichokuwa paani mwa nyumba yake, akaumia vibaya. Kwa hiyo akawatuma wajumbe, akawaambia, “Nendeni kwa Baal-zebubu, mungu wa mji wa Ekroni, mkamwulize kama nitapona ugonjwa huu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ahazia akaanguka dirishani penye chumba chake cha juu mle Samaria, akapata kuugua; ndipo, alipotuma wajumbe, aliowaambia: Nendeni kumwuliza Baali-Zebubu, mungu wa Ekroni, kama nitapona ugonjwa huu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Ahazia akaanguka katika dirisha la chumba chake orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Ahazia alipokuwa Samaria alianguka kutoka chumba kilichokuwa juu ya paa ya nyumba yake, akaumia vibaya. Kwa hiyo akawatuma wajumbe, akawaambia: “Muende kwa Bali-Zebubu, mungu wa muji wa Ekuroni, mumwulize kama nitapona ugonjwa huu.”