2 Kings 1:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia nabii Elia kutoka Tishbe, aende kukutana na wajumbe hao na kuwauliza, “Kwa nini mnakwenda kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Je, hakuna Mungu nchini Israeli?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini malaika wa Mwenyezi Mungu akamwambia Ilya Mtishbi, “Panda uende ukakutane na wajumbe wa mfalme wa Samaria, uwaulize, ‘Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ndiyo maana mnaenda kumuuliza Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni?’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini malaika wa Bwana akamwambia Eliya Mtishbi, Ondoka, uende ukaonane na wale wajumbe wa mfalme wa Samaria, ukawaambie, Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia nabii Elia kutoka Tishbe, aende kukutana na wajumbe hao na kuwauliza, “Kwa nini mnakwenda kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Je, hakuna Mungu nchini Israeli?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini malaika wa BWANA akamwambia Eliya, Mtishbi, “Panda ukakutane na wajumbe wa mfalme wa Samaria na uwaulize, ‘Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ndiyo maana mnakwenda kumwuliza Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni?’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini malaika wa bwana akamwambia Ilya, Mtishbi, “Panda ukakutane na wajumbe wa mfalme wa Samaria, uwaulize, ‘Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ndiyo maana mnakwenda kumuuliza Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni?’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini malaika wa BWANA akamwambia Eliya Mtishbi, Ondoka, uende ukaonane na wale wajumbe wa mfalme wa Samaria, ukawaambie, Je! Ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia nabii Elia kutoka Tishbe, aende kukutana na wajumbe hao na kuwauliza, “Kwa nini mnakwenda kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Je, hakuna Mungu nchini Israeli?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini malaika wa Bwana akamwambia Elia wa Tisibe: Inuka, uwaendee wajumbe wa mfalme wa Samaria, uwaambie: Je? Kwao Waisiraeli hakuna Mungu, ninyi mkienda kumwuliza Baali-Zebubu, mungu wa Ekroni?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini malaika wa BWANA akamwambia Eliya Mtishbi, Ondoka, uende ukaonane na wale wajumbe wa mfalme wa Samaria, ukawaambie, Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini malaika wa Yawe akamwambia nabii Elia wa muji wa Tisibe, aende kukutana na wajumbe hao na kuwauliza: “Kwa nini munakwenda kwa Bali-Zebubu, mungu wa Ekuroni? Hakuna Mungu katika inchi ya Israeli?