2 Kings 1:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakamjibu, “Tumekutana na mtu ambaye alitutuma turudi kukuambia kwamba Mwenyezi-Mungu amesema hivi: ‘Kwa nini unatuma wajumbe kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Je, hakuna Mungu nchini Israeli? Hutashuka katika kitanda ulichokipanda; bali hakika utakufa!’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamjibu, “Mtu mmoja alikuja kukutana nasi, naye akatuambia, ‘Rudini kwa mfalme aliyewatuma na mkamwambie, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ndiyo maana unawatuma watu kwenda kuuliza kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni? Kwa hiyo hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!” ’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamwambia, Mtu alitokea, akaonana nasi, akatuambia, Enendeni, rudini kwa mfalme yule aliyewatuma, mkamwambie, Bwana asema hivi Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Basi kwa ajili ya hayo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakamjibu, “Tumekutana na mtu ambaye alitutuma turudi kukuambia kwamba Mwenyezi-Mungu amesema hivi: ‘Kwa nini unatuma wajumbe kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Je, hakuna Mungu nchini Israeli? Hutashuka katika kitanda ulichokipanda; bali hakika utakufa!’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamjibu, “Mtu fulani alikuja kukutana nasi, naye akatuambia, ‘Rudini kwa mfalme aliyewatuma na mwambieni, “Hili ndilo asemalo BWANA: Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ndiyo maana unawatuma watu kwenda kuuliza kwa Baal-Zebubu, aliye mungu wa Ekroni? Kwa hiyo hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!” ’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamjibu, “Mtu fulani alikuja kukutana nasi, naye akatuambia, ‘Rudini kwa mfalme aliyewatuma na mkamwambie, “Hili ndilo asemalo bwana: Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ndiyo maana unawatuma watu kwenda kuuliza kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni? Kwa hiyo hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!” ’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamwambia, Mtu alitokea, akaonana nasi, akatuambia, Nendeni, rudini kwa mfalme yule aliyewatuma, mkamwambie, BWANA asema hivi Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Basi kwa ajili ya hayo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakamjibu, “Tumekutana na mtu ambaye alitutuma turudi kukuambia kwamba Mwenyezi-Mungu amesema hivi: ‘Kwa nini unatuma wajumbe kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Je, hakuna Mungu nchini Israeli? Hutashuka katika kitanda ulichokipanda; bali hakika utakufa!’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamwambia: Mtu ametujia, akatuambia: Haya! Rudini kwa mfalme aliyewatuma, mmwambie: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Je? Kwao Waisiraeli hakuna Mungu, wewe ukituma kumwuliza Baali-Zebubu, mungu wa Ekroni? Kwa sababu hii hutaondoka tena hapo kitandani, unapolala, ila utakufa kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamwambia, Mtu alitokea, akaonana nasi, akatuambia, Enendeni, rudini kwa mfalme yule aliyewatuma, mkamwambie, BWANA asema hivi Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Basi kwa ajili ya hayo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamujibu: “Tumekutana na mutu ambaye alitutuma turudi kukuambia kwamba Yawe amesema hivi: ‘Kwa nini unatuma wajumbe kwa Bali-Zebubu, mungu wa Ekuroni? Hakuna Mungu katika inchi ya Israeli? Hautashuka katika kitanda ulichopanda juu yake. Hakika utakufa.’ ”