2 Kings 10:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na Yehu akapeleka habari katika nchi yote ya Israeli ili wafuasi wote wa Baali wahudhurie kila mmoja. Wakaja wote na kujaa katika hekalu la Baali kutoka pembe moja mpaka nyingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Yehu akapeleka ujumbe katika Israeli yote, nao watumishi wote wa Baali wakaja, hakuna hata mmoja ambaye hakufika. Wakasongamana ndani ya hekalu la Baali hadi likajaa tangu mlango hadi mwisho wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yehu akatuma wajumbe katika Israeli yote, nao wote waliomwabudu Baali wakaja, wala hakusalia mtu ye yote asiyekuja. Wakaingia nyumbani mwa Baali; ikajaa nyumba ya Baali tangu mlango hata mlango.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na Yehu akapeleka habari katika nchi yote ya Israeli ili wafuasi wote wa Baali wahudhurie kila mmoja. Wakaja wote na kujaa katika hekalu la Baali kutoka pembe moja mpaka nyingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akapeleka ujumbe katika Israeli yote na watumishi wote wa Baali wakaja, hakuna hata mmoja ambaye hakufika. Wakasongana ndani ya hekalu la Baali mpaka likajaa tangu mwanzo hadi mwisho wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Yehu akapeleka ujumbe katika Israeli yote, nao watumishi wote wa Baali wakaja, hakuna hata mmoja ambaye hakufika. Wakasongana ndani ya hekalu la Baali hadi likajaa tangu mlango hadi mwisho wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yehu akatuma wajumbe katika Israeli yote, nao wote waliomwabudu Baali wakaja, wala hakusalia mtu yeyote asiyekuja. Wakaingia nyumbani mwa Baali; ikajaa nyumba ya Baali tangu mlango hata mlango.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na Yehu akapeleka habari katika nchi yote ya Israeli ili wafuasi wote wa Baali wahudhurie kila mmoja. Wakaja wote na kujaa katika hekalu la Baali kutoka pembe moja mpaka nyingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yehu akatuma kwa Waisiraeli wote, wakaja wote waliomtumikia Baali, hakusalia hata mmoja asiyekuja. Kisha wakaingia nyumbani mwa Baali, nayo hiyo nyumba ya Baali ikajaa watu huku na huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yehu akatuma wajumbe katika Israeli yote, nao wote waliomwabudu Baali wakaja, wala hakusalia mtu ye yote asiyekuja. Wakaingia nyumbani mwa Baali; ikajaa nyumba ya Baali tangu mlango hata mlango.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na Yehu akapeleka habari katika inchi yote ya Israeli kusudi wafuasi wote wa Bali wahuzurie kila mumoja. Wakakuja wote na kujaa katika hekalu la Bali kutoka pembe moja mpaka nyingine.