2 Kings 10:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akaingia pamoja na Yehonadabu kumtolea Baali matambiko na tambiko za kuteketezwa. Yehu alikuwa ameweka watu themanini nje ya hekalu na kuwapa maagizo haya: ‘Waueni watu hawa wote. Yeyote atakayemwacha hata mmoja wao atoroke atalipa kwa maisha yake!’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo wakaingia ndani ili kutoa kafara na sadaka ya kuteketezwa. Wakati huu, Yehu alikuwa amewaweka watu wake themanini akiwa amewapa onyo kwamba, “Ikiwa mmoja wenu atamwachia mtu yeyote ninayemweka mikononi mwenu atoroke, itakuwa uhai wako kwa uhai wake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaingia ili watoe dhabihu na sadaka za kuteketezwa. Basi Yehu alikuwa amejiwekea nje watu themanini, akasema, Mtu mmoja akiokoka wa watu niliowatia mikononi mwenu, amwachaye huyo, roho yake itakuwa badala ya roho yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akaingia pamoja na Yehonadabu kumtolea Baali matambiko na tambiko za kuteketezwa. Yehu alikuwa ameweka watu themanini nje ya hekalu na kuwapa maagizo haya: ‘Waueni watu hawa wote. Yeyote atakayemwacha hata mmoja wao atoroke atalipa kwa maisha yake!’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo wakaingia ndani ili kutoa kafara na sadaka ya kuteketezwa. Wakati huu, Yehu alikuwa amewaweka watu wake themanini akiwa amewapa onyo kwamba, “Ikiwa mmoja wenu atamwachia mtu ye yote ninayemweka mikononi mwake atoroke, itakuwa uhai wako kwa uhai wake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo wakaingia ndani ili kutoa kafara na sadaka ya kuteketezwa. Wakati huu, Yehu alikuwa amewaweka watu wake themanini akiwa amewapa onyo kwamba, “Ikiwa mmoja wenu atamwachia mtu yeyote ninayemweka mikononi mwake atoroke, itakuwa uhai wako kwa uhai wake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaingia ili watoe dhabihu na sadaka za kuteketezwa. Basi Yehu alikuwa amejiwekea nje watu themanini, akasema, Mtu mmoja akiokoka wa watu niliowatia mikononi mwenu, amwachaye huyo, roho yake itakuwa badala ya roho yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akaingia pamoja na Yehonadabu kumtolea Baali matambiko na tambiko za kuteketezwa. Yehu alikuwa ameweka watu themanini nje ya hekalu na kuwapa maagizo haya: ‘Waueni watu hawa wote. Yeyote atakayemwacha hata mmoja wao atoroke atalipa kwa maisha yake!’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakaja kutoa vipaji vya tambiko na ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima. Lakini Yehu alikuwa amejiwekea nje watu 80, akawaambia: Mtu atakayepona kwao hao, nitakaowaleta na kuwatia mikononi mwenu, basi, roho yake itakuwa mahali pa roho yake yule.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaingia ili watoe dhabihu na sadaka za kuteketezwa. Basi Yehu alikuwa amejiwekea nje watu themanini, akasema, Mtu mmoja akiokoka wa watu niliowatia mikononi mwenu, amwachaye huyo, roho yake itakuwa badala ya roho yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akaingia pamoja na Yonadabu kwa kumutolea Bali matoleo na sadaka za kuteketezwa. Yehu alikuwa ameweka watu makumi tatu inje ya hekalu na kuwapa maagizo haya: “Muwaue watu hawa wote. Yeyote atakayemwacha hata mumoja wao atoroke atalipa kwa maisha yake!”