2 Kings 10:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo ofisa mkuu wa nyumba ya mfalme na ofisa mkuu wa mji, wakishirikiana na viongozi wengine na walinzi, wakampelekea Yehu ujumbe huu: “Sisi tu watumwa wako, na tuko tayari kufanya lolote unalosema. Lakini hatutamtawaza mtu yeyote kuwa mfalme; fanya unavyoona vyema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi msimamizi wa jumba la mfalme, mtawala wa mji, na wazee na walezi wakatuma ujumbe huu kwa Yehu: “Sisi tu watumishi wako, na tutafanya kila kitu utakachosema. Hatutamteuwa mtu yeyote kuwa mfalme. Wewe fanya uonalo kuwa ni bora.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha yeye aliyekuwa juu ya nyumba, na yeye aliyekuwa juu ya mji, na wazee, na walezi, wakatuma ujumbe kwa Yehu, wakisema, Sisi tu watumwa wako, kila neno utakalotuambia, tutalifanya; hatutamfanya mtu awaye yote kuwa mfalme; ufanye yaliyo mema machoni pako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo ofisa mkuu wa nyumba ya mfalme na ofisa mkuu wa mji, wakishirikiana na viongozi wengine na walinzi, wakampelekea Yehu ujumbe huu: “Sisi tu watumwa wako, na tuko tayari kufanya lolote unalosema. Lakini hatutamtawaza mtu yeyote kuwa mfalme; fanya unavyoona vyema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi msimamizi wa jumba la kifalme, mtawala wa mji, wazee na walezi wakatuma ujumbe huu kwa Yehu: “Sisi tu watumishi wako na tutafanya kila kitu utakachosema. Hatutamteuwa mtu ye yote kuwa mfalme, wewe fanya uonalo kuwa ni bora.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi msimamizi wa jumba la mfalme, mtawala wa mji, na wazee na walezi wakatuma ujumbe huu kwa Yehu: “Sisi tu watumishi wako, na tutafanya kila kitu utakachosema. Hatutamteuwa mtu yeyote kuwa mfalme. Wewe fanya uonalo kuwa ni bora.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha yeye aliyekuwa juu ya nyumba, na yeye aliyekuwa juu ya mji, na wazee, na walezi, wakatuma ujumbe kwa Yehu, wakisema, Sisi tu watumwa wako, kila neno utakalotuambia, tutalifanya; hatutamfanya mtu awaye yote kuwa mfalme; ufanye yaliyo mema machoni pako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo ofisa mkuu wa nyumba ya mfalme na ofisa mkuu wa mji, wakishirikiana na viongozi wengine na walinzi, wakampelekea Yehu ujumbe huu: “Sisi tu watumwa wako, na tuko tayari kufanya lolote unalosema. Lakini hatutamtawaza mtu yeyote kuwa mfalme; fanya unavyoona vyema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo wale waliousimamia ule mlango na mji pamoja na wazee na watunzaji wa wana wakatuma kwa Yehu kumwambia: Sisi tu watumwa wako, nayo yote, utakayotuagiza, tutayafanya, lakini hatuwezi kumweka mtu kuwa mfalme; fanya tu yaliyo mema machoni pako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha yeye aliyekuwa juu ya nyumba, na yeye aliyekuwa juu ya mji, na wazee, na walezi, wakatuma ujumbe kwa Yehu, wakisema, Sisi tu watumwa wako, kila neno utakalotuambia, tutalifanya; hatutamfanya mtu awaye yote kuwa mfalme; ufanye yaliyo mema machoni pako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo mukubwa wa nyumba ya mufalme na musimamizi wa muji, wakishirikiana na viongozi wengine na walinzi, wakamupelekea Yehu ujumbe huu: “Sisi ni watumwa wako, na tuko tayari kufanya lolote unalosema. Lakini hatutamuweka mutu yeyote kuwa mufalme. Fanya unavyotaka.”