2 Kings 10:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mtumishi mmoja akamwendea na kusema, “Vichwa vya wana wa mfalme vimekwisha letwa.” Ndipo akaamuru, “Viwekwe chini katika mafungu mawili kwenye lango la mji; halafu viache vikae huko mpaka asubuhi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mjumbe alipofika, akamwambia Yehu, “Wameleta vichwa vya wana wa mfalme.” Ndipo Yehu akaagiza, “Viwekeni malundo mawili katika ingilio la lango la mji hadi asubuhi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaja mjumbe, akamwambia, akasema, Wamevileta vile vichwa vya wana wa mfalme. Akasema, Viwekeni chungu mbili penye maingilio ya lango hata asubuhi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mtumishi mmoja akamwendea na kusema, “Vichwa vya wana wa mfalme vimekwisha letwa.” Ndipo akaamuru, “Viwekwe chini katika mafungu mawili kwenye lango la mji; halafu viache vikae huko mpaka asubuhi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mjumbe alipofika, akamwambia Yehu, “Wameleta vichwa vya wana wa mfalme.” Ndipo Yehu akaagiza, “Viwekeni katika marundo mawili katika ingilio la lango la mji mpaka asubuhi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mjumbe alipofika, akamwambia Yehu, “Wameleta vichwa vya wana wa mfalme.” Ndipo Yehu akaagiza, “Viwekeni malundo mawili katika ingilio la lango la mji mpaka asubuhi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaja mjumbe, akamwambia, akasema, Wamevileta vile vichwa vya wana wa mfalme. Akasema, Viwekeni marundo mawili penye maingilio ya lango hata asubuhi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha mtumishi mmoja akamwendea na kusema, “Vichwa vya wana wa mfalme vimekwisha letwa.” Ndipo akaamuru, “Viwekwe chini katika mafungu mawili kwenye lango la mji; halafu viache vikae huko mpaka asubuhi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mjumbe alipokwenda kumpasha habari, ya kuwa wamevileta vichwa vya wana wa mfalme, akasema: Viwekeni machungu mawili hapo pa kuingia langoni mwa mji mpaka kesho!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaja mjumbe, akamwambia, akasema, Wamevileta vile vichwa vya wana wa mfalme. Akasema, Viwekeni chungu mbili penye maingilio ya lango hata asubuhi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mutumishi mumoja akamwendea na kusema: “Vichwa vya wana wa mufalme vimekwisha kuletwa.” Halafu akaamuru: “Muviweke chini katika mafungu mawili kwenye mulango wa muji, muviache vikae kule mpaka asubui.”