2 Kings 10:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Asubuhi yake akatoka, akasimama na kuwaambia watu wote, “Nyinyi ni waadilifu, angalia mimi nilikula njama dhidi ya bwana wangu na kumuua. Lakini ni nani aliyewaua hawa wote?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kesho yake asubuhi, Yehu akatoka nje. Akasimama mbele ya watu wote na akasema, “Hamna hatia. Ni mimi niliyepanga njama dhidi ya bwana wangu na kumuua, lakini ni nani aliyewaua wote hawa?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa asubuhi, akatoka, akasimama, akawaambia watu wote, Ninyi ni wenye haki; tazameni, mimi nalifanya fitina juu ya bwana wangu, nikamwua; ila ni nani aliyewapiga hawa wote?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Asubuhi yake akatoka, akasimama na kuwaambia watu wote, “Nyinyi ni waadilifu, angalia mimi nilikula njama dhidi ya bwana wangu na kumuua. Lakini ni nani aliyewaua hawa wote?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Asubuhi yake, Yehu akatoka nje. Akasimama mbele ya watu wote na akasema, “Hamna hatia. Ni mimi niliyefanya shauri baya dhidi ya bwana wangu na kumwua, lakini ni nani aliyewaua wote hawa?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Asubuhi yake, Yehu akatoka nje. Akasimama mbele ya watu wote na akasema, “Hamna hatia. Ni mimi niliyefanya shauri baya dhidi ya bwana wangu na kumuua, lakini ni nani aliyewaua wote hawa?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa asubuhi, akatoka, akasimama, akawaambia watu wote, Ninyi ni wenye haki; tazameni, mimi nalimfitinia bwana wangu, nikamwua; ila ni nani aliyewapiga hawa wote?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Asubuhi yake akatoka, akasimama na kuwaambia watu wote, “Nyinyi ni waadilifu, angalia mimi nilikula njama dhidi ya bwana wangu na kumuua. Lakini ni nani aliyewaua hawa wote?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, alipotoka asubuhi akasimama hapo, akawaambia watu wote: Ninyi hamna kosa lo lote. Nitazameni mimi! Mimi nimemlia bwana wangu njama, nikamwua. Lakini aliyewaua hawa wote ni nani?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa asubuhi, akatoka, akasimama, akawaambia watu wote, Ninyi ni wenye haki; tazameni, mimi nalifanya fitina juu ya bwana wangu, nikamwua; ila ni nani aliyewapiga hawa wote?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Asubui yake akatoka, akasimama na kuwaambia watu wote: “Ninyi ni watu wa haki. Mimi nilifanya mupango wa kuasi bwana wangu na kumwua. Lakini ni nani aliyewaua hawa wote?