2 Kings 11:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu akamtoa nje mwana wa mfalme, akamvika taji kichwani, na kumpa ule ushuhuda; wakamtawaza na kumpaka mafuta; wakapiga makofi na kusema, “Aishi mfalme!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yehoyada akamtoa mwana wa mfalme na kumvika taji, akampa nakala ya agano, na kumtangaza kuwa mfalme. Wakampaka mafuta, nao watu wakapiga makofi na kupaza sauti, wakisema, “Mfalme aishi maisha marefu!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo akamleta nje mwana wa mfalme, akamvika taji, na kumpa ushuhuda; wakamfanya mfalme, wakamtia mafuta; wakapiga makofi, wakasema, mfalme na aishi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu akamtoa nje mwana wa mfalme, akamvika taji kichwani, na kumpa ule ushuhuda; wakamtawaza na kumpaka mafuta; wakapiga makofi na kusema, “Aishi mfalme!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yehoyada akamtoa mwana wa mfalme na kumvika taji, akampa nakala ya agano na kumtangaza kuwa mfalme. Wakamtia mafuta, nao watu wakapiga makofi na kupaza sauti wakisema, “Mfalme aishi maisha marefu!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yehoyada akamtoa mwana wa mfalme na kumvika taji, akampa nakala ya agano, na kumtangaza kuwa mfalme. Wakamtia mafuta, nao watu wakapiga makofi na kupaza sauti, wakisema, “Mfalme aishi maisha marefu!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo akamleta nje mwana wa mfalme, akamvika taji, na kumpa ushuhuda; wakamfanya mfalme, wakamtia mafuta; wakapiga makofi, wakasema, Mfalme na aishi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu akamtoa nje mwana wa mfalme, akamvika taji kichwani, na kumpa ule ushuhuda; wakamtawaza na kumpaka mafuta; wakapiga makofi na kusema, “Aishi mfalme!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akamtoa mwana wa mfalme, akamvika kilemba cha kifalme, wakampa nacho kizingo cha Ushahidi, wakamfanya kuwa mfalme wakimpaka mafuta. Kisha wakapiga makofi na kusema: Pongezi, mfalme!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo akamleta nje mwana wa mfalme, akamvika taji, na kumpa ushuhuda; wakamfanya mfalme, wakamtia mafuta; wakapiga makofi, wakasema, mfalme na aishi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yehoyada akamutoa inje mwana wa mufalme, akamuvalisha taji juu ya kichwa, na kumupa maandiko ya sheria. Wakamuweka kuwa mufalme na kumupakaa mafuta. Wakapiga mikono na kusema: “Mufalme aishi milele!”