2 Kings 11:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha kuhani Yehoyada akaamuru makapteni wa jeshi akisema; “Mtoeni nje katikati ya askari, na ueni mtu yeyote atakayemfuata.” Kwa sababu kuhani alisema, “Asiuawe katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani Yehoyada akawaamuru majemadari wa vikosi vya mamia, waliokuwa viongozi wa jeshi, “Mtoeni nje kati ya safu, na mkamuue kwa upanga yeyote anayemfuata.” Kwa kuwa kuhani alikuwa amesema, “Hatauawa ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yehoyada kuhani akawaamuru wakuu wa mamia, majemadari wa jeshi, akawaambia, Mtoeni kati ya safu; naye ye yote amfuataye mwueni kwa upanga. Kwani kuhani akasema, Asiuawe nyumbani mwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha kuhani Yehoyada akaamuru makapteni wa jeshi akisema; “Mtoeni nje katikati ya askari, na ueni mtu yeyote atakayemfuata.” Kwa sababu kuhani alisema, “Asiuawe katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani Yehoyada akawaagiza majemadari wa vikosi vya mamia, waliokuwa wasimamizi wa jeshi, “Mleteni huyo Athalia nje katikati ya safu, na mtieni upanga mtu ye yote atakayemfuata.” Kwa kuwa kuhani alikuwa amesema, “Hatauawa ndani ya Hekalu la BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani Yehoyada akawaagiza majemadari wa vikosi vya mamia, waliokuwa viongozi wa jeshi, “Mleteni nje kati ya safu, na mkamuue kwa upanga yeyote anayemfuata.” Kwa kuwa kuhani alikuwa amesema, “Hatauawa ndani ya Hekalu la bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yehoyada kuhani akawaamuru wakuu wa mamia, majemadari wa jeshi, akawaambia, Mtoeni kati ya safu; naye yeyote amfuataye mwueni kwa upanga. Kwani kuhani akasema, Asiuawe nyumbani mwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha kuhani Yehoyada akaamuru makapteni wa jeshi akisema; “Mtoeni nje katikati ya askari, na ueni mtu yeyote atakayemfuata.” Kwa sababu kuhani alisema, “Asiuawe katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mtambikaji Yoyada alipowaagiza wakuu wa mamia waliovisimamia vikosi, akawaambia: Mtoeni hapa penye mipango ya watu! Naye atakayemfuata na auawe kwa upanga! Kwani mtambikaji alisema, asiuawe Nyumbani mwa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yehoyada kuhani akawaamuru wakuu wa mamia, majemadari wa jeshi, akawaambia, Mtoeni kati ya safu; naye ye yote amfuataye mwueni kwa upanga. Kwani kuhani akasema, Asiuawe nyumbani mwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha kuhani Yehoyada akaamuru wakubwa wa waaskari akisema: “Mumwondoshe inje katikati ya waaskari, na muue mutu yeyote atakayemufuata.” Kwa sababu kuhani alisema: “Asiuawe katika nyumba ya Yawe.”