2 Kings 11:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya Mwenyezi-Mungu na mfalme na watu kwamba watakuwa watu wa Mwenyezi-Mungu; kadhalika alifanya agano kati ya mfalme na watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya Mwenyezi Mungu na mfalme na watu kwamba watakuwa watu wa Mwenyezi Mungu. Akafanya pia agano kati ya mfalme na watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha, Yehoyada akafanya mapatano kati ya Bwana na mfalme na watu, ili wawe watu wa Bwana; tena kati ya mfalme na watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya Mwenyezi-Mungu na mfalme na watu kwamba watakuwa watu wa Mwenyezi-Mungu; kadhalika alifanya agano kati ya mfalme na watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yehoyada akafanya Agano kati ya BWANA na mfalme na watu kwamba watakuwa watu wa BWANA. Akafanya pia agano kati ya mfalme na watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya bwana na mfalme na watu kwamba watakuwa watu wa bwana. Akafanya pia agano kati ya mfalme na watu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha, Yehoyada akafanya mapatano kati ya BWANA na mfalme na watu, ili wawe watu wa BWANA; tena kati ya mfalme na watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya Mwenyezi-Mungu na mfalme na watu kwamba watakuwa watu wa Mwenyezi-Mungu; kadhalika alifanya agano kati ya mfalme na watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yoyada akafanya agano na Bwana, yeye na mfalme wa watu, wawe ukoo wake Bwana; agano jingine akamfanyia mfalme na watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha, Yehoyada akafanya mapatano kati ya BWANA na mfalme na watu, ili wawe watu wa BWANA; tena kati ya mfalme na watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya Yawe na mufalme na watu kwamba watakuwa watu wa Yawe. Vilevile alifanya agano kati ya mufalme na watu.