2 Kings 11:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu wakazi wote wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuibomoa, wakavunja madhabahu pamoja na sanamu zake, hata wakamuua Matani, kuhani wa Baali mbele ya madhabahu. Kuhani Yehoyada akaweka walinzi kulinda nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wote wa nchi wakaenda kwenye hekalu la Baali na kulibomoa. Wakavunjavunja madhabahu na sanamu, na kumuua Matani kuhani wa Baali mbele ya hayo madhabahu. Kisha Yehoyada kuhani akawaweka walinzi kwenye Hekalu la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wote wa nchi wakaiendea nyumba ya Baali, wakaiangusha; madhabahu zake na sanamu zake wakazivunja-vunja kabisa, na Matani kuhani wa Baali wakamwua mbele ya madhabahu. Na Yehoyada kuhani akaweka maakida juu ya nyumba ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu wakazi wote wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuibomoa, wakavunja madhabahu pamoja na sanamu zake, hata wakamuua Matani, kuhani wa Baali mbele ya madhabahu. Kuhani Yehoyada akaweka walinzi kulinda nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wote wa nchi wakaenda kwenye hekalu la Baali na kulibomoa. Wakavunja madhabahu zote na sanamu vipande vipande na kumwua Matani kuhani wa Baali mbele ya hiyo madhabahu. Kisha Yehoyada kuhani akawaweka walinzi kwenye Hekalu la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wote wa nchi wakaenda kwenye hekalu la Baali na kulibomoa. Wakavunjavunja madhabahu na sanamu, na kumuua Matani kuhani wa Baali mbele ya hayo madhabahu. Kisha Yehoyada kuhani akawaweka walinzi kwenye Hekalu la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wote wa nchi wakaiendea nyumba ya Baali, wakaiangusha; madhabahu zake na sanamu zake wakazivunjavunja kabisa, na Matani kuhani wa Baali wakamwua mbele ya madhabahu. Na Yehoyada kuhani akaweka walinzi wa nyumba ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu wakazi wote wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuibomoa, wakavunja madhabahu pamoja na sanamu zake, hata wakamuua Matani, kuhani wa Baali mbele ya madhabahu. Kuhani Yehoyada akaweka walinzi kulinda nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, watu wote wa nchi hiyo walipoiingia nyumba ya Baali, wakaibomoa, nazo meza za kumtambikia na vinyago vyake wakavivunjavunja kabisa, naye Matani, mtambikaji wa Baali, wakamwua mbele ya meza za kutambikia. Kisha yule mtambikaji akaweka wakaguzi wa Nyumba ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wote wa nchi wakaiendea nyumba ya Baali, wakaiangusha; madhabahu zake na sanamu zake wakazivunja-vunja kabisa, na Matani kuhani wa Baali wakamwua mbele ya madhabahu. Na Yehoyada kuhani akaweka maakida juu ya nyumba ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu wakaaji wakaenda kwenye nyumba ya Bali na kuibomoa, wakavunja mazabahu pamoja na sanamu zake, hata wakamwua Matani, kuhani wa Bali mbele ya mazabahu. Kuhani Yehoyada akaweka walinzi kwa kulinda nyumba ya Yawe.