2 Kings 11:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliwachukua makapteni, Wakari na wakazi wote; nao wakamsindikiza mfalme kutoka nyumba ya Mwenyezi-Mungu wakapitia katika lango la walinzi mpaka ikulu. Naye akakikalia kiti cha enzi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pamoja naye akawachukua majemadari wa mamia, Wakari, walinzi na watu wote wa nchi, nao kwa pamoja wakamteremsha mfalme kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu na kwenda kwenye jumba la mfalme, wakiingilia njia ya lango la walinzi. Ndipo mfalme akachukua nafasi yake kwenye kiti cha ufalme;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawatwaa wakuu wa mamia, na Wakari, na walinzi, na watu wote wa nchi; wakamleta mfalme kushuka nyumbani mwa Bwana, wakaja kwa njia ya mlango wa walinzi mpaka nyumba ya mfalme. Naye akakaa katika kiti cha enzi cha wafalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliwachukua makapteni, Wakari na wakazi wote; nao wakamsindikiza mfalme kutoka nyumba ya Mwenyezi-Mungu wakapitia katika lango la walinzi mpaka ikulu. Naye akakikalia kiti cha enzi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pamoja naye akawachukua majemadari wa mamia, Wakari, walinzi na watu wote wa nchi, nao kwa pamoja wakamshusha mfalme kutoka katika Hekalu la BWANA na kwenda kwenye jumba la kifalme, wakiingilia njia ya lango la walinzi. Ndipo mfalme akachukua nafasi yake kwenye kiti cha enzi,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pamoja naye akawachukua majemadari wa mamia, Wakari, walinzi na watu wote wa nchi, nao kwa pamoja wakamteremsha mfalme kutoka Hekalu la bwana na kwenda kwenye jumba la mfalme, wakiingilia njia ya lango la walinzi. Ndipo mfalme akachukua nafasi yake kwenye kiti cha enzi,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawatwaa wakuu wa mamia, na Wakari, na walinzi, na watu wote wa nchi; wakamleta mfalme kushuka nyumbani mwa BWANA, wakaja kwa njia ya mlango wa walinzi mpaka nyumba ya mfalme. Naye akakaa katika kiti cha enzi cha wafalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aliwachukua makapteni, Wakari na wakazi wote; nao wakamsindikiza mfalme kutoka nyumba ya Mwenyezi-Mungu wakapitia katika lango la walinzi mpaka ikulu. Naye akakikalia kiti cha enzi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akawachukua wakuu wa mamia nao askari nao wapiga mbio pamoja na watu wote wa nchi hii, wakamtoa mfalme Nyumbani mwa Bwana, wakaingia nyumbani mwa mfalme na kushika njia ya lango la wapiga mbio; ndivyo, alivyopata kukaa katika kiti cha kifalme cha wafalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawatwaa wakuu wa mamia, na Wakari, na walinzi, na watu wote wa nchi; wakamleta mfalme kushuka nyumbani mwa BWANA, wakaja kwa njia ya mlango wa walinzi mpaka nyumba ya mfalme. Naye akakaa katika kiti cha enzi cha wafalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliwakamata wakubwa wa waaskari, waaskari walinzi na watu wote, nao wakamusindikiza mufalme kutoka nyumba ya Yawe, wakapitia katika mulango wa walinzi mpaka kwenye nyumba ya kifalme. Naye mufalme akakiikalia kiti cha kifalme.