2 Kings 11:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini katika mwaka wa saba Yehoyada alituma ujumbe na kuwakusanya makapteni wa Wakari na walinzi; akaamuru wamjie katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, naye akafanya nao mapatano na kuwaapisha humo katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Halafu akawaonesha Yoashi mwana wa mfalme Ahazia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa saba, Yehoyada akatumania wakuu wa vikundi vya mamia, na Wakari na walinzi, nao wakaletwa kwake katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Alifanya agano nao na kuwaapisha katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Ndipo akawaonesha mwana wa mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata mwaka wa saba Yehoyada akatuma, na kuwaleta wakuu wa mamia, wa Wakari, na wa walinzi, akawaleta kwake ndani ya nyumba ya Bwana; akapatana nao, akawaapisha nyumbani mwa Bwana, akawaonyesha huyo mwana wa mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini katika mwaka wa saba Yehoyada alituma ujumbe na kuwakusanya makapteni wa Wakari na walinzi; akaamuru wamjie katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, naye akafanya nao mapatano na kuwaapisha humo katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Halafu akawaonesha Yoashi mwana wa mfalme Ahazia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa saba Yehoyada kuhani akaamuru waletwe wakuu wa vikundi vya mamia wa Wakari na walinzi, nao wakaletwa kwake kwenye Hekalu la BWANA. Akafanya agano nao na kuwaapisha katika Hekalu la BWANA. Ndipo akawaonyesha mwana wa mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa saba, Yehoyada akatumania wakuu wa vikundi vya mamia, na Wakari, na walinzi, nao wakaletwa kwake katika Hekalu la bwana. Alifanya agano nao na kuwaapisha katika Hekalu la bwana. Ndipo akawaonyesha mwana wa mfalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata mwaka wa saba Yehoyada akatuma, na kuwaleta wakuu wa mamia, wa Wakari, na wa walinzi, akawaleta kwake ndani ya nyumba ya BWANA; akapatana nao, akawaapisha nyumbani mwa BWANA, akawaonesha huyo mwana wa mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini katika mwaka wa saba Yehoyada alituma ujumbe na kuwakusanya makapteni wa Wakari na walinzi; akaamuru wamjie katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, naye akafanya nao mapatano na kuwaapisha humo katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Halafu akawaonesha Yoashi mwana wa mfalme Ahazia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwaka wa saba Yoyada akatuma kuwachukua wakuu wa mamia ya askari na wapiga mbio, akawapeleka kwake Nyumbani mwa Bwana, akafanya maagano nao akiwaapisha mle Nyumbani. Kisha akawaonyesha mwana wa mfalme,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata mwaka wa saba Yehoyada akatuma, na kuwaleta wakuu wa mamia, wa Wakari, na wa walinzi, akawaleta kwake ndani ya nyumba ya BWANA; akapatana nao, akawaapisha nyumbani mwa BWANA, akawaonyesha huyo mwana wa mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini katika mwaka wa saba Yehoyada alituma ujumbe na kuwakusanya wakubwa wa waaskari na walinzi. Akaamuru wamufikie katika nyumba ya Yawe, naye akafanya nao mapatano na kuwaapisha humo katika nyumba ya Yawe. Halafu akawaonyesha Yoasi mwana wa mufalme Ahazia.