2 Kings 11:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akatoa amri: “Mtafanya hivi: Mtakapokuja kushika zamu siku ya Sabato, theluthi moja italinda ikulu;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaamuru akisema, “Hivi ndivyo iwapasavyo kufanya: Ninyi ambao mko makundi matatu mnaoingia zamu siku ya Sabato, theluthi moja italinda jumba la kifalme,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaamuru, akasema, Hili ndilo neno mtakalolifanya; theluthi yenu, mtakaoingia siku ya sabato, mtayalinda malinzi ya nyumba ya mfalme;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akatoa amri: “Mtafanya hivi: mtakapokuja kushika zamu siku ya Sabato, theluthi moja italinda ikulu;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaamuru akisema, “Hivi ndivyo iwapasavyo kufanya: Ninyi ambao mko makundi matatu mnaokwenda zamu siku ya Sabato, theluthi yenu itakuwa ikilinda jumba la kifalme,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaamuru akisema, “Hivi ndivyo iwapasavyo kufanya: Ninyi ambao mko makundi matatu mnaoingia zamu siku ya Sabato, theluthi yenu inayolinda jumba la kifalme,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaamuru, akasema, Hili ndilo neno mtakalolifanya; theluthi yenu, mtakaoshika zamu siku ya sabato, mtalinda nyumba ya mfalme;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akatoa amri: “Mtafanya hivi: Mtakapokuja kushika zamu siku ya Sabato, theluthi moja italinda ikulu;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akawaagiza kwamba: Hili ndilo neno, mtakalolifanya: fungu lenu la tatu watakaoingia kazi siku ya mapumziko na walinde ulinzi wa nyumba ya mfalme;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaamuru, akasema, Hili ndilo neno mtakalolifanya; theluthi yenu, mtakaoingia siku ya sabato, mtayalinda malinzi ya nyumba ya mfalme;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akatoa amri: “Mutafanya hivi: mutakapokuja kushika zamu siku ya Sabato, sehemu moja ya tatu italinda nyumba ya kifalme,