2 Kings 11:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtamzunguka mfalme, kila mtu na silaha yake mkononi na mtu yeyote atakayethubutu kuwakaribia lazima auawe. Lazima mkae na mfalme, awe anatoka au anakaa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jipangeni kumzunguka mfalme, kila mtu akiwa na silaha yake mkononi. Yeyote anayesogelea safu zenu lazima auawe. Kaeni karibu na mfalme popote aendapo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtamzunguka mfalme pande zote, kila mtu mwenye silaha zake mkononi; naye awaye yote aingiaye ndani ya safu auawe; mkafuatane na mfalme, akitoka na akiingia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtamzunguka mfalme, kila mtu na silaha yake mkononi na mtu yeyote atakayethubutu kuwakaribia lazima auawe. Lazima mkae na mfalme, awe anatoka au anakaa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jipangeni kumzunguka mfalme, kila mtu akiwa na silaha yake mkononi mwake. Ye yote anayesogelea safu yenu ya askari ni lazima auawe. Kaeni karibu na mfalme po pote aendako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jipangeni kumzunguka mfalme, kila mtu akiwa na silaha yake mkononi. Yeyote anayesogelea safu zenu lazima auawe. Kaeni karibu na mfalme popote aendapo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtamzunguka mfalme pande zote, kila mtu mwenye silaha zake mkononi; naye awaye yote aingiaye ndani ya safu auawe; mkafuatane na mfalme, akitoka na akiingia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtamzunguka mfalme, kila mtu na silaha yake mkononi na mtu yeyote atakayethubutu kuwakaribia lazima auawe. Lazima mkae na mfalme, awe anatoka au anakaa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sharti mmzunguke mfalme pande zote kila mtu akiyashika mata yake, kila atakayeingia katika hii mipango ya watu na auawe! Hivyo sharti mwe na mfalme, akitoka, hata akiingia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtamzunguka mfalme pande zote, kila mtu mwenye silaha zake mkononi; naye awaye yote aingiaye ndani ya safu auawe; mkafuatane na mfalme, akitoka na akiingia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutamuzunguka mufalme, kila mutu na silaha yake katika mukono na mutu yeyote atakayesubutu kuwakaribia mumwue. Mukae na mufalme, ikiwa anatoka au anaikaa.”