2 Kings 11:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makapteni walitii amri zote alizotoa kuhani Yehoyada. Kila ofisa akawachukua watu wake wote, wale waliokuwa wamemaliza zamu na wale waliokuwa wanaingia kushika zamu siku ya Sabato, basi wakamwendea kuhani Yehoyada.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakuu wa vikosi vya mamia wakafanya vile kuhani Yehoyada aliagiza. Kila mmoja akawachukua watu wake, wale waliokuwa wakiingia zamu siku ya Sabato na wale waliokuwa wakienda mapumziko, nao wakaja kwa kuhani Yehoyada.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakuu wa mamia wakafanya sawasawa na yote aliyowaamuru Yehoyada kuhani; wakawatwaa kila mtu watu wake, hao watakaoingia sabato, nao watakaotoka sabato, wakaja kwa Yehoyada kuhani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makapteni walitii amri zote alizotoa kuhani Yehoyada. Kila ofisa akawachukua watu wake wote, wale waliokuwa wamemaliza zamu na wale waliokuwa wanaingia kushika zamu siku ya Sabato, basi wakamwendea kuhani Yehoyada.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Majemadari wa vikosi vya mamia wakafanya sawasawa kama alivyoagiza kuhani Yehoyada. Kila mmoja akawachukua watu wake, wale waliokuwa wakienda zamu siku ya Sabato na wale waliokuwa katika mapumziko, nao wakaja kwa kuhani Yehoyada.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakuu wa vikosi vya mamia wakafanya kama vile kuhani Yehoyada aliagiza. Kila mmoja akawachukua watu wake, wale waliokuwa wakiingia zamu siku ya Sabato na wale waliokuwa wakienda mapumziko, nao wakaja kwa kuhani Yehoyada.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakuu wa mamia wakafanya sawasawa na yote aliyowaamuru Yehoyada kuhani; wakawatwaa kila mtu watu wake, hao watakaoingia sabato, nao watakaotoka sabato, wakaja kwa Yehoyada kuhani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makapteni walitii amri zote alizotoa kuhani Yehoyada. Kila ofisa akawachukua watu wake wote, wale waliokuwa wamemaliza zamu na wale waliokuwa wanaingia kushika zamu siku ya Sabato, basi wakamwendea kuhani Yehoyada.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakuu wa mamia wakayafanya yote, kama mtambikaji Yoyada alivyowaagiza; kila mtu akawachukua watu wake walioingia kazi siku ya mapumziko nao waliotoka kazi siku ya mapumziko, wakaja kwa mtambikaji Yoyada.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakuu wa mamia wakafanya sawasawa na yote aliyowaamuru Yehoyada kuhani; wakawatwaa kila mtu watu wake, hao watakaoingia sabato, nao watakaotoka sabato, wakaja kwa Yehoyada kuhani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa walitii amri zote kuhani Yehoyada alizotoa. Kila mukubwa akakamata watu wake wote, wale waliokuwa wamemaliza zamu na wale waliokuwa wanaingia kushika zamu siku ya Sabato, basi wakamwendea kuhani Yehoyada.