2 Kings 12:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila walipoona kuwa mna fedha nyingi sandukuni, katibu wa mfalme na kuhani mkuu waliingia na kuhesabu na kuzifunga katika vifurushi fedha zote zilizopatikana katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mara walipoona kuwa kuna kiasi kikubwa cha fedha ndani ya kisanduku, mwandishi wa mfalme na kuhani mkuu walikuja, wakazihesabu fedha hizo zilizoletwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, na kuziweka katika mifuko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, walipoona ya kuwa fedha nyingi imo kashani, karani wa mfalme akapanda na kuhani mkuu, wakaifunga mifukoni, wakaihesabu fedha iliyoonekana nyumbani mwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila walipoona kuwa mna fedha nyingi sandukuni, katibu wa mfalme na kuhani mkuu waliingia na kuhesabu na kuzifunga katika vifurushi fedha zote zilizopatikana katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mara walipoona kuwa kuna kiasi kikubwa cha fedha ndani ya kisanduku, mwandishi wa jumba la kifalme na Kuhani Mkuu walikuja, wakazihesabu fedha hizo zilizoletwa katika Hekalu la BWANA na kuziweka katika mifuko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mara walipoona kuwa kuna kiasi kikubwa cha fedha ndani ya kisanduku, mwandishi wa mfalme na kuhani mkuu walikuja, wakazihesabu fedha hizo zilizoletwa katika Hekalu la bwana, na kuziweka katika mifuko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, walipoona ya kuwa fedha nyingi imo kashani, karani wa mfalme akapanda na kuhani mkuu, wakaifunga mifukoni, wakaihesabu fedha iliyoonekana nyumbani mwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila walipoona kuwa mna fedha nyingi sandukuni, katibu wa mfalme na kuhani mkuu waliingia na kuhesabu na kuzifunga katika vifurushi fedha zote zilizopatikana katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipoona, ya kuwa fedha zimo nyingi mle kashani, mwandishi wa mfalme na mtambikaji mkuu wakapanda, wakazifunga na kuzihesabu fedha zote zilizooneka Nyumbani mwa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, walipoona ya kuwa fedha nyingi imo kashani, karani wa mfalme akapanda na kuhani mkuu, wakaifunga mifukoni, wakaihesabu fedha iliyoonekana nyumbani mwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yehoyada akatwaa sanduku na kutoboa tundu kwenye kifuniko chake, kisha akaliweka kwenye mazabahu upande wa kuume, mutu anapoingia katika nyumba ya Yawe. Nao makuhani waliokuwa wakichunga kwenye mulango waliweka ndani ya sanduku feza zote zilizotolewa katika nyumba ya Yawe.