2 Kings 12:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini pesa hizo hazikutumiwa kwa kulipia utengenezaji wa mabirika ya fedha, mikasi ya kukatia tambi za mishumaa, mabakuli, tarumbeta, wala kwa vyombo vingine vyovyote vya dhahabu au vya fedha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Fedha zilizoletwa kwenye Hekalu hazikutumiwa kutengenezea masinia ya fedha, mikasi ya kusawazishia tambi, mabakuli ya kunyunyizia, tarumbeta wala vyombo vingine vyovyote vya dhahabu au fedha kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini havikufanywa kwa nyumba ya Bwana vikombe vya fedha, wala makasi, wala mabakuli, wala panda, wala vyombo vyo vyote vya dhahabu, wala vyombo vya fedha, kwa hiyo fedha iliyoletwa nyumbani mwa Bwana;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini pesa hizo hazikutumiwa kwa kulipia utengenezaji wa mabirika ya fedha, mikasi ya kukatia tambi za mishumaa, mabakuli, tarumbeta, wala kwa vyombo vingine vyovyote vya dhahabu au vya fedha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Fedha zilizoletwa kwenye Hekalu hazikutumiwa kutengenezea masinia ya fedha, mikasi ya kusawazishia tambi, mabakuli ya kunyunyizia, tarumbeta wala vyombo vingine vyo vyote vya dhahabu au fedha kwa ajili ya Hekalu la BWANA;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Fedha zilizoletwa kwenye Hekalu hazikutumiwa kutengenezea masinia ya fedha, mikasi ya kusawazishia tambi, mabakuli ya kunyunyizia, tarumbeta wala vyombo vingine vyovyote vya dhahabu au fedha kwa ajili ya Hekalu la bwana;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini havikufanywa kwa nyumba ya BWANA vikombe vya fedha, wala makasi, wala mabakuli, wala panda, wala vyombo vyovyote vya dhahabu, wala vyombo vya fedha, kwa hiyo fedha iliyoletwa nyumbani mwa BWANA;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini pesa hizo hazikutumiwa kwa kulipia utengenezaji wa mabirika ya fedha, mikasi ya kukatia tambi za mishumaa, mabakuli, tarumbeta, wala kwa vyombo vingine vyovyote vya dhahabu au vya fedha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mabakuli ya fedha na makato ya kusafishia mishumaa na vyano na matarumbeta na vyombo vyo vyote vya dhahabu na vya fedha vya kutumiwa Nyumbani mwa Bwana havikutengenezwa kwa zile fedha zilizoletwa Nyumbani mwa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini havikufanywa kwa nyumba ya BWANA vikombe vya fedha, wala makasi, wala mabakuli, wala panda, wala vyombo vyo vyote vya dhahabu, wala vyombo vya fedha, kwa hiyo fedha iliyoletwa nyumbani mwa BWANA;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kwa wajengaji na wenye kuchonga mawe, na zikatumiwa kwa kununua mbao na mawe yaliyochongwa kwa kutengeneza nyumba ya Yawe na kutimiza mahitaji mengine yote ya kazi ya kutengeneza nyumba.