2 Kings 12:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoashi mfalme wa Yuda alichukua sadaka zote zilizowekwa wakfu na babu zake wafalme wa Yuda: Yehoshafati, Yehoramu na Ahazia, na kuongeza zile zake, pamoja na dhahabu yote iliyokuwa katika hazina ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu na katika ikulu, akazituma kwa Hazaeli mfalme wa Aramu. Naye Hazaeli akatoka Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Yoashi mfalme wa Yuda akavichukua vyombo vyote vitakatifu vilivyowekwa wakfu na baba zake, yaani Yehoshafati, Yehoramu na Ahazia, wafalme wa Yuda, na vyombo vyake vyote ambavyo alikuwa ameviweka wakfu, pamoja na dhahabu yote iliyokuwa katika hazina za Hekalu la Mwenyezi Mungu na katika jumba la kifalme; akazipeleka kwa Hazaeli mfalme wa Aramu, ambaye hatimaye aliondoka Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yoashi mfalme wa Yuda akavitwaa vyote alivyoviweka wakfu Yehoshafati, na Yehoramu, na Ahazia, baba zake, wafalme wa Yuda, navyo vyote alivyoweka wakfu mwenyewe, na dhahabu yote iliyoonekana katika hazina za nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme, akamletea Hazaeli mfalme wa Shamu; basi akaenda zake kutoka Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoashi mfalme wa Yuda alichukua sadaka zote zilizowekwa wakfu na babu zake wafalme wa Yuda: Yehoshafati, Yehoramu na Ahazia, na kuongeza zile zake, pamoja na dhahabu yote iliyokuwa katika hazina ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu na katika ikulu, akazituma kwa Hazaeli mfalme wa Aramu. Naye Hazaeli akatoka Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Yoashi mfalme wa Yuda akavichukua vyombo vyote vitakatifu vilivyowekwa wakfu na baba zake, yaani Yehoshafati, Yehoramu na Ahazia wafalme wa Yuda, zawadi ambazo yeye mwenyewe alikuwa ameziweka wakfu pamoja na dhahabu yote iliyokutwa katika hazina za Hekalu la BWANA na katika jumba la kifalme, akazipeleka kwa Hazaeli mfalme wa Aramu, ambaye hatimaye aliondoka Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Yoashi mfalme wa Yuda akavichukua vyombo vyote vitakatifu vilivyowekwa wakfu na baba zake, yaani Yehoshafati, Yehoramu na Ahazia, wafalme wa Yuda, zawadi ambazo yeye mwenyewe alikuwa ameziweka wakfu pamoja na dhahabu yote iliyokutwa katika hazina za Hekalu la bwana na katika jumba la kifalme, akazipeleka kwa Hazaeli mfalme wa Aramu, ambaye hatimaye aliondoka Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yoashi mfalme wa Yuda akavitwaa vyote alivyoviweka wakfu Yehoshafati, na Yehoramu, na Ahazia, baba zake, wafalme wa Yuda, navyo vyote alivyoweka wakfu mwenyewe, na dhahabu yote iliyoonekana katika hazina za nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, akamletea Hazaeli mfalme wa Shamu; basi akaenda zake kutoka Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoashi mfalme wa Yuda alichukua sadaka zote zilizowekwa wakfu na babu zake wafalme wa Yuda: Yehoshafati, Yehoramu na Ahazia, na kuongeza zile zake, pamoja na dhahabu yote iliyokuwa katika hazina ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu na katika ikulu, akazituma kwa Hazaeli mfalme wa Aramu. Naye Hazaeli akatoka Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Yoasi, mfalme wa Wayuda, alipovichukua vipaji vitakatifu vyote, Yosafati na Yoramu na Ahazia walivyovitoa, viwe mali za Bwana, na vipaji vitakatifu, alivyovitoa yeye, nazo dhahabu zote zilizopatikana katika vilimbiko vya Nyumba ya Bwana namo katika vilimbiko vya nyumba ya mfalme, akampelekea Hazaeli, mfalme wa Ushami; ndipo, alipoondoka Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yoashi mfalme wa Yuda akavitwaa vyote alivyoviweka wakfu Yehoshafati, na Yehoramu, na Ahazia, baba zake, wafalme wa Yuda, navyo vyote alivyoweka wakfu mwenyewe, na dhahabu yote iliyoonekana katika hazina za nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, akamletea Hazaeli mfalme wa Shamu; basi akaenda zake kutoka Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo Hazaeli mufalme wa Aramu akaushambulia muji wa Gati na kuuteka. Lakini Hazaeli alipoelekea Yerusalema kusudi aushambulie,